Saturday 27th, April 2024
@KIBITI TOWN
Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti inategemea kuupokea Mwenge wa Uhuru,Uwanja wa ndege Dar es Salaam ukitokea Wilaya ya Mafia.
Katika Halmashauri ya Wilaya Kibiti Mwenge wa Uhuru Utapokelewa katika viwanja vya Shule ya Sekondari Mjawa,ambapo Kiongozi wa Mbio za Mwenge
Kitaifa atatembelea jumla ya miradi 7 ya maendeleo , miradi 2 itazinduliwa,miradi 3 itawekewa jiwe la msingi na miradi 2 itafanyiwa ukaguzi.Aidha Mwenge wa Uhuru Utaendelea na mbio
zake ndani ya Halmashauri na utafanya mkesha katika viwanja vya Kibiti stendi.Mwenge wa uhuru utakabidhiwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji tarehe 3/6/2017
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.