Majukumu ya Idara ya Afya
Kusimamia shughuli zote za utoaji wa huduma za Afya kwa kufuata miongozo na sera za afya na ubora unaohitajika ,pamoja na kutoa ushauri wa kitaalamu kuhusu masuala yote yahusuyo afya kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.
Kuandaa Mpango kabambe wa Afya wa mwaka na kutoa taarifa za utekelezaji wa shughuli za afya kama zilivyo ainishwa katika Mpango na kuziwasilisha katika mamlaka husika.
Kufanya ziara za usimamizi na ufuatiliaji wa utaoji wa huduma za afya katika vituo vyote vya kutolea huduma za afya katika Wilaya.
Kusimamia usambazaji wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi katika vituo vyote vya huduma Wilayani na kuhakikisha dawa zinakuwepo vituoni.
Kubuni na kutayarisha mikakati ya kuinua ubora wa huduma ya Afya.
Kutoa huduma za outreach na mobile kliniki katika kuboresha utoaji wa huduma za Afya.
Kusimamia watumishi wa Afya na kuhakikisha kuwa wanafanya kazi kwa kuzingatia maadili ya kazi, kanuni na miongozo mbalimbali zinazosimamia utendaji wa watumishi,
Kusimamia rasilimali na nyenzo za kuendesha huduma zote za Afya na kuzitunza.
Kuhamasisha jamii kuchangia huduma za Afya na kushiriki katika kampeni mbalimbali za Afya.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.