Majukumu ya Idara ya Elimu Sekondari
9.1: Malengo
Halmashauri ya Wilaya ya kibaha ina jumla ya shule za Sekondari 13, ambapo shule 8 ni za Serikali na 5 ni za Binafsi. Idara ya Elimu Sekondari imeendelea kuratibu shughuli mbalimbali za Elimu kama ifuatavyo;
UTEKELEZAJI ELIMU SEKONDARI
Shule 02 za kidato cha Tano na Sita zimeanzishwa kwenye Tarafa ya Mlandizi na Soga ambazo ni Kilangalanga na Rafsanjan Soga.
Utekelezaji
9.2: Hali Ya Maendeleo Ya Elimu
Nyumba zimejengwa Kwala na Ruvu Station (02)
Utekelezaji
Kuendelea na mpango wa ujenzi wa Nyumba za walimu hasa sehemu za vijijini.
Ujenzi wa Jengo la Utawala – Kilangalanga (01)
Ujenzi wa Mabwalo – Kilangalanga (01)
Kujenga vyoo – Dossa, Kilangalanga, Mihande (MMES II)
Kutengeneza madawati
Kukarabati Madarasa, Dosa Azizi, Mihande (Miradi ya Benki ya Dunia) MMES II
Kujenga madarasa – Shule ya Sekondari Kilangalanga (04 ya kidato cha 5na 6)
Utekelezaji
Kusimamia ubora wa miundombinu ya Shule za Sekondari na kuleta ufanisi katika utoaji wa elimu.
Shule zote zinashiriki michezo ya UMMISETA kuanzia ngazi ya shule hadi Taifa na kimataifa (UMMISETA & FEASA)
Utekelezaji
Kuimarisha michezo shuleni
Maabara zimejengwa kwa kila Shule na zinatosheleza uhitaji kwa sasa
Utekelezaji
Kuendeleza mpango wa kujenga Maabara
Hosteli zimejengwa
Idadi ya walimu imeongezeka
Vitabu na vifaa vya maabara vimenunuliwa kupitia fedha za uendeshaji hadi sasa uwiano ni 1.1 (Hisabati na Sayansi na 1:3 Lugha na Sanaa).
Utekelezaji
Idadi ya wanafunzi wanaoandikishwa kila mwaka imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka, mfano mwaka 2010 jumla ya wanafunzi 993 kati yao wavulana ni 505 na wasichana ni 488 waliandikishwa, ambapo kwa Januari, 2015 wanafunzi walioandikishwa ni 1,058 ambao kati yao wavulana ni 484 na wasichana ni 574, ongezeko hili ni sawa na 7%.
Uandikishaji wanafunzi wa Kidato cha kwanza
Katika kipindi cha mwaka 2005 hadi 2010 kulikuwa na maabara 06 tu kati ya 24 zilizokuwa zinahitajika katika ufundishaji wa masomo ya sayansi. Hadi Juni, 2015 jumla ya maabara 24 zimepatikana kati ya hizo, maabara 07 zipo katika hatua mbalimbali za ukamilishaji.
Ufaulu umekuwa ukiongezeka mwaka hadi mwaka kama inavyoonekana katika majedwali yafuatayo;
NA
|
MWAKA |
UFAULU % |
1
|
2012 |
54 |
2
|
2013 |
41 |
3
|
2014 |
91 |
5
|
2015 |
89.5 |
NA |
MWAKA |
UFAULU % |
1
|
2012 |
81.5 |
2
|
2013 |
88.1 |
3
|
2014 |
96.5 |
4
|
2015 |
95.8 |
(c) KIDATO CHA VI
NA |
MWAKA |
UFAULU % |
1
|
2010 |
38.8 |
2
|
2011 |
33.5 |
3
|
2012 |
21.5 |
4
|
2013 |
38.9 |
5
|
2014 |
65.2 |
6
|
2015 |
68.2 |
Hadi mwaka 2010 Halmashauri ilikuwa na shule 1 tu yenye kidato cha V na VI. Lakini kwasasa Halmashauri ina shule 3 zenye kidato cha V na VI.
Katika kipindi cha mwaka 2005 hadi 2010 nyumba za walimu zilikuwa 45, lakini hadi kufikia 2015 nyumba za walimu zilizokamilika zipo 48 kati ya hizo nyumba 02 zipo hatua mbalimbali za ujenzi.
Katika kipindi cha mwaka 2005 hadi 2010 Halmashauri ilikuwa na walimu 195, hadi 2015 idadi ya waalimu katika Halmashauri imeongezeka hadi 308 ambayo ni sawa 58%.
Katika kipindi cha mwaka 2005 hadi 2010 Halmashauri ilikuwa na hosteli 15, kufikia 2015 Halmashauri ina jumla ya hosteli 20. Sawa na ongezeko la 33.3%.
Halmashauri imefanikiwa kuongeza idadi ya matundu ya vyoo hadi kufikia 150 kutoka 127 ya mwaka 2010 ambayo ni sawa na ongezeko la 18.1%.
Katika kipindi cha mwaka 2005 hadi 2010 Shule za Serikali zilikuwa na madawati na meza 3,641, hadi kufikia 2015 shule za Serikali zina jumla ya madawati na meza 4,500. Sawa na ongezeko la 24%.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.