Kuwakilisha Wizara ya Elimu na TAMISEMI katika ngazi zote
Kufafanua na kusimamia utekelezaji wa sera ya Elimu , sheria na kanuni katika Elimu ya watu wazima na ufundi stadi
Kutoa ushauri wa kitaalamu kwa Halmashauri ya wilaya kuhusu masuala yote ya kielimu.
Kudhibiti matumizi ya fedha za Elimu kwa mujibu wa miongozo ya fedha za serikali.
Kushughulikia upanuzi wa Elimu katika ngazi ya Elimu ya Awali, Elimu ya Msingi, Elimu ya Watu Wazima, mafunzo ya Ualimu na vituo vya ufundi stadi.
Kufuatilia kwa madhumuni ya kutathmini maendeleo ya Elimu katika wilaya.
Kutayarisha na kusimamia utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya Elimu kila mwaka.
Kuhakikisha kwamba shule zote zinaboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia.
Kuhimiza udhibiti na na nidhamu ya walimu na wanafunzi wilayani.
Kusimamia maslahi ya walimu
Kuratibu na kusimamia mitihani ya darasa la Pili, la Nne na la Saba , mafunzo ya ualimu na mitihani ya vituo vya ufundi stadi katika wilaya kwa kushirikiana na uongozi wa Mkoa na Baraza la Mitihani la Tanzania.
Kufuatilia utekelezaji wa taarifa za ukagizi wa shule na vyuo.
Kusimamia maendeleo ya Taaluma na michezo katika wilaya.
Kukusanya, kuratibu na kuchambua takwimu za Elimu katika wilaya kwa ajili ya Mipango ya Maendeleo katika ngazi ya shule, wilaya, mkoa na Taifa.
Ni Katibu wa Kamati ya Elimu ya Halmashauri ya Wilaya kufuatana na kifungu cha 2 cha sheria Na. 25 ya mwaka 1978 na kurekebishwa mwaka 1995.
UTEKELEZAJI ELIMU MSINGI
Katika kipindi cha mwaka 2005 hadi 2015 idara ya elimu msingi illitekeleza miradi miwili mikubwa yenye thamani ya Tsh. 109,190,800. Fedha hizo ni Ruzuku ya maendeleo kutoka serikali kuu kupitia Mpango wa maendeleo ya elimu ya msingi (MMEM). Katika mwaka 2007/2008 Idara ya elimu ilipokea jumla ya Tshs. 16,500,000.000 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba 3 vya madarasa Tshs. 9,300,000.000 na nyumba 2 za walimu Tshs. 7,200,000.00 kwa mwaka 2011/2012 tsh. 32,690,800.00 zilitolewa na serikali kwa ajili ya ukamilishaji wa vyumba 3 vya madarasa Tsh. 13,790,800,Tsh2,500,000.00 ni fedha za madawati 73, kujenga matundu 4 ya vyoo kwa tsh. 2,400,000.00 na Tshs. 14,000,000.00 ujenzi wa nyumba ya mwalimu kwa mwaka 2013/2014 idara ilipokea tsh. 20,000,000.00 za umaliziaji wa chumba kimoja cha darasa katika shule ya msingi uhuru.
Mwaka 2009/2010, idara ya elimu msingi ilipokea kiasi cha tsh 40,000,000.00 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha watoto wenye ulemavu kilichopo katika shule ya msingi Mlandizi .Ktai ya fedha hizo Tsh. 19,980,000.00 zilitumika katika ujenzi wa vyumba 3 vya madarasa ya watoto wenye ulemavu, Tshs. 7,050,000.000 ujenzi wa uzio wa madarsa ,Tsh, 9,513,000.00 zilitumika kujenga matundu 5 ya vyoo na Tsh, 3,457,000.00 zilitumika kutengeneza samani za shule kwa ajili ya wnafunzi wenye ulemavu.
Aidha, katika kutekeleza miradi hiyo mikubwa miwili idara ya elimu msingi imeweza kupunguza msongamano uliokuwa umejitokeza katika shule kubwa za jirani na shule ya Uhuru za Mtongani na Azimio .Pia katika shule ya watoto wenye ulemavu mradi umeweza kuwaweka pamoja watoto wenye ulemavu katika kituo kimoja.