Mujukumu ya Idara ya Fedha na Biashara
Kushauri Halmashauri juu ya masuala yote ya fedha.
Kuandaa bajeti ya mwaka ya mapato na matumizi kwa kushirikiana na Afisa mipango na wakuu wengine wa Idara.
Kutengeneza na kutunza mfumo bora wa kihasibu na utunzaji mzuri wa nyaraka mbalimbali za fedha.
Kuandaa taarifa za hali halisi ya mapato na matumizi kulingana na bajeti ya mwaka na kutoa mapendekezo juu ya kiwango kilichopo cha mapato na matumizi.
Kuandaa taarifa mbalimbali za fedha kwa ajili ya kuziwasilisha kwenye vikao vya waheshimiwa madiwani.
Kuhakikisha kunakuwepo na mfumo mzuri wa ndani wa usimamizi na uandishi wa nyaraka na taratibu zote za fedha.
Kuandaa na kuwasilisha taratibu zote za fedha kwenye kamati ya fedha na utawala ili iidhinishwe na kuzigawa kwa wakuu wote wa Idara.
Kusimamia mali zote za Halmashauri na masuala yote yanayohusu usimamizi wa fedha za Halmashauri,
Kusimamia ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri kama bajeti ilivyopitishwa.
Kuhakikisha kuwa hesabu za Halmashauri zinafungwa na kuwasilishwa kwa mkaguzi wa nje (NAO).
3.2: Mapato Kwa Kipindi cha Miaka Mitano 2010/11 Hadi 2014/15
Hali ya ukusanyaji wa mapato katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha kwa kipindi cha mwaka 2010/2011 hadi 2014/2015 ni kama ifuatavyo;
JEDWALI NA. 3: MAKISIO NA MAPATO HALISI
Mwaka |
Makiso |
Halisi |
Asilimia |
2010/2011
|
8,908,536,196.45 |
8,521,287,175.34 |
95.7 |
2011/2012
|
12,285,893,490.80 |
7,897,856,661.20 |
64.2 |
2012/2013
|
15,795,484,546.04 |
12,204,235,952.50 |
77.26 |
2013/2014
|
12,818,766,900.00 |
13,090,484,088.64 |
108 |
2014/2015
|
22,595,394,348.55 |
16,595,724,192.50 |
75 |
Chanzo; Idara ya Fedha
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.