Utangulizi
Wilaya ya Kibiti ni mpya iliyogawanywa kutoka Wilaya ya Rufiji na kutangazwa katika Gazeti la Serikali (GN) Na. 433 B. la tarehe 25/09/2015 na kuanza kutekeleza majukumu yake mwaka wa fedha 2016/2017.
Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti ipo Mashariki ya Tanzania Bara katika ukanda wa Pwani ya bahari ya Hindi. Wilaya ina eneo la ukubwa wa kilometa za mraba 3,854 sawa na asilimia 11.4 ya eneo lote la Mkoa wa Pwani.
Wilaya imepakana na Wilaya ya Mkuranga upande wa kaskazini, Upande wa Kaskazini magharibi imepakana na Wilaya ya Kisarawe, Wilaya ya Mafia na Bahari ya Hindi – upande wa Mashariki, Wilaya za Kilwa na Rufiji – upande wa Kusini. (Ramani hapo chini) .
Ramani ya Kibiti
Wilaya ya Kibiti ni miongoni mwa Wilaya Saba (7) zinazounda Mkoa wa Pwani. Kiutawala Wilaya imeundwa na Halmashauri 1, Jimbo la uchaguzi 1, tarafa 3 (Mbwera, Kikale na Kibiti) , Mamlaka ya Mji Mdogo 1, Kata 16, Vijiji 58 na Vitongoji 269. (Tazama jedwali Na. 1).
Jedwali Na. 01: Maeneo ya Kiutawala Wilaya ya Kibiti
S/N
|
Tarafa
|
Idadi ya Kata Kata
|
Idadi ya Vijiji
|
Idadi ya Vitongoji
|
1
|
Mbwera
|
4
|
12
|
55
|
2
|
Kibiti
|
9
|
33
|
161
|
3
|
Kikale
|
3
|
13
|
53
|
|
Jumla
|
16
|
58
|
269
|
Kwa mujibu wa Sensa ya watu na makazi iliyofanyika mwaka 2012, Wilaya ilikuwa ina jumla ya watu 122,648 (Wanaume 59,168 na Wanawake 63,480).
Kwa kasi ya ongezeko la watu kwa asilimia 1.9, maoteo ya mwaka 2022, Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti inakadiriwa kufikia watu 147,048 (wanaume 71,422 na wanawake 76,626).
Jedwali Na. 02: Idadi ya Watu Kikata.
Na.
|
KATA
|
IDADI YA WATU KWA JINSIA
|
KAYA
|
|||
Wanaume
|
Wanawake
|
Jumla
|
Idadi
|
Wastani
|
||
1 | Kibiti
|
7,150
|
8,006
|
15,156
|
3,597
|
4.2
|
2 | Bungu
|
8,884
|
9,835
|
18,719
|
4,101
|
4.6
|
3 | Mahege
|
2,831
|
3,137
|
5,968
|
1,347
|
4.4
|
4 | Mchukwi
|
3,411
|
3,590
|
7,001
|
1,601
|
4.4
|
5 | Dimani
|
2,701
|
2,744
|
5,445
|
1,251
|
4.4
|
6 | Mtawanya
|
3,251
|
3,521
|
6,772
|
1,469
|
4.6
|
7 | Mjawa
|
5,606
|
6,439
|
12,045
|
2,726
|
4.4
|
8 | Mlanzi
|
2,549
|
2,667
|
5,216
|
1,119
|
4.7
|
9 | Mwambao
|
2,662
|
2,520
|
5,182
|
1,241
|
4.2
|
10 | Mtunda
|
3,998
|
4,137
|
8,135
|
1,685
|
4.8
|
11 | Ruaruke
|
3,450
|
3,779
|
7,229
|
1,642
|
4.4
|
12 | Salale
|
4,462
|
4,614
|
9,076
|
1,817
|
4.8
|
13 | Mbuchi
|
2,992
|
3,033
|
6,025
|
1,366
|
4.4
|
14 | Kiongoroni
|
2,433
|
2,463
|
4,896
|
1,085
|
4.5
|
15 | Maparoni
|
1,062
|
1,145
|
2,207
|
501
|
4.5
|
16 | Msala
|
1,726
|
1,850
|
3,576
|
790
|
4.5
|
|
Jumla
|
59,168
|
63,480
|
122,648
|
27,338
|
4.4
|
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.