Majukumu ya Idara ya Mifugo na Uvuvi
• Kubuni mipango ya uzalishaji mifugo.
• Kuratibu mipango ya ugani kuhusiana na mifugo.
• Kuratibu na kuendesha mafunzo ya ufugaji bora, usindikaji wa mazao ya mifugo kwa wataalu wa mifugo na wafugaji.
• Kubuni, kuanzisha na kutekeleza miradi ya maendeleo ya mifugo.
• Kutafiti maeneo mapya yanayofaa kwa ufugaji wa mifugo mbalimbali.
• Kufanya utafiti juu ya uihalibifu wa mazingira.
• Kushiriki katika shughuli za kudhibiti milipuko ya wanyama na viumbe waharibifu wa malisho.
• Kuandaa taarifa ya robo, nusu na mwaka juu ya maendeleo ya mifugo.
• Kufuatilia, kuweka, kuchambua na kutafsiri takwimu za uzalishaji wa mifugo.
• Kusimamia huduma zote za afya ya mifugo afya ya umma na wanyama.
• Kuandaa mipango ya muda mfupi na mrefu ya kudhibiti na kutokomeza magonjwa ya wanyama.
• Kukusanya, kuchambua, kuhifadhi, kusambaza na kutumia data za magonjwa ya mifugona taarifa nyingine.
• Kuratibu matumizi ya maji ya mifugo na uhifadhi wa maeneo ya malisho na vyanzo vya maji.
• Kuelimisha wafugaji juu ya matumizi bora ya nyanda za malisho.
• Kusimamia utekelezaji wa sheria za nyanda za malisho na vyanzo uzalishaji wa vyakula vya mifugo. • Kuhamasisha utunzaji na uhifadhi wa nyanda za malisho kwa mbinu za asili.
• Kuelimisha na kuhamasisha matumizi ya mabaki ya mazao na masalia ya mazao.
• Kupunguza migogoro kati wafanya biashara wakubwa wa binadamu na wazalishaji wa vyakula vya mifugo.
• Kusajili na kusimia sekta binafsi za mifugo.
• Kuhamasisha sekta binafsi kuwekeza katika uzalishaji wa nyama na ngozi.
• Kusimamia utekelezaji wa sheria ya mifugo na sheria ya ngozi.
• Kuhamasisha uzalishaji, ukusanyaji na utunzaji na uuzaji wa ngozi bora.
• Kuongeza thamani ya ngozi.
• Kutoa mafunzo kwa wadau mbalimbali wa ngozi.
• Kuhamasisha matumizi ya masoko bora ya mifugo.
• Kutekeleza sera ya uvuvi.
• Uhifadhi wa samaki na viumbe wengine wa majini na mazingira yao.
• Kuratibu na kusimamia uhifadhi wa mazingira.
• Kuendeleza uvunaji endelevu wa samaki na viumbe wengine wa baharini, maziwa, mito, mabwawa na malambo.
• Kutoa ushauri wa kitaalam kuhusu uvuvi bora, utengenezaji na uhifadhi bora wa samakina mazao ya uvuvi, biashara na masoko ya samaki pamoja ufugaji wa samaki na viumbe wengine wa majini.
• Kutoa leseni za uvuvi.
• Kuendesha mafunzo ya taaluma ya uvuvi.
• Kusimamia na kutekeleza sharia za uvuvi (k.m kuzuia uvuvi haramu).
• Kusimamia ukusanyaji wa takwimu za uvuvi pamoja na maduhuli.
• Kuratibu shughuli za utafiti wa uvuvi.
• Kutoa ushauri na mafunzo kwa wananchi juu ta uendelezaji na matumizi enelevu ya rasilimali za uvuvi.
• Kukagua ubora wa samaki na mazao ya uvuvi na kuweka viwango vya kitaifa.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.