29.11.2023.
Afisa Utumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti Bw. Msena Bina ametoa mafunzo ya mfumo wa kupima utendaji kazi kwa watumishi na taasisi kwa njia ya mtandao (PEPMIS) kwa Watendaji wa Kata waliopo chini ya idara ya Utumishi wilayani humo.
Akitoa mafunzo hayo katika aukumbi wa Halmshauri Bw. Bina amewasisitiza watendaji kusikiliza kwa umakini ili waweze kuelewa wanachojifunza, kwani mfumo huo ni mpya na unatakiwa kuanza kutumika ifikapo disemba 30 mwaka huu.
Vilevile Afisa Utumishi huyo amesema kwamba, mpaka sasa tayari watumishi wamekwishajisajili kwenye mfumo huo, kwa ajili ya kuingiza shughuli zote zilizopo (activities) watakazokuwa wakitekeleza katika mpango kazi wa 2023/24.
Aidha, tarehe 24 na 27 mwezi Novemba mafunzo hayo yalifanyika kwa Wakuu wa Idara na Vitengo pamoja na Wakuu wa sehemu katika Idara.
Nao baadhi ya Watendaji Kata walioshiriki mafunzo hayo wamesema mfumo utawasaidia kuongeza Ari na kasi ya utendaji kwani ni mfumo unaowapima watumishi namna wanavyotekeleza majukumu yao ya kila siku. Pia mfumo huo utawapunguzia safari za kwenda Wilayani kufuatilia baadhi ya huduma kwani kazi zote zitafanyika kwa njia ya mtandao kama vile kujaza Opras, masuala ya mikopo, uhamisho, upandishwaji wa madaraja na malipo ya mishahara yao.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.