Benki ya Azania Tanzania imeitembelea Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti na viunga vyake kutoa elimu na kubainisha huduma wanazozitoa kwa wafanyakazi.
Akikaribisha ugeni huo Afisa Utumishi wa wilaya ya Kibiti Msena Bina aliwataka watumishi wote kusikiliza kwa makini elimu inayotolewa ili iweze kutumika pindi itakapohitajika hususani kuongeza nguvu ya kufanya maendeleo kwa kupata mikopo kutoka benki ya Azania .
Wakiwa katika ukumbi wa Halmashauri Afisa Uhusiano Neema Erasto amesema, Benki ya Azania imeingia makubaliano na utawala wa Halmashauri ya Kibiti kudhamini watumishi watakaohitaji mkopo kupitia mishahara yao na mkopo huo hutolewa kulingana na kiwango cha mshahara wa mtumishi.
“Hii ni benki ya serikali ni benki ya wazawa, karibuni tuwahudumie tunatoa mikopo ya aina mbalimbali”Alisema Neema .
Vilevile Neema amesema Benki yao inatoa huduma mbalimbali za kibenki kwa upande wa wafanyakazi inatoa huduma ya bima ya wafanyakazi (consumer loan) na bima ya ujumla (Insurance) inajumuisha bima za nyumba, ajali ya moto, magari, kilimo na afya pia mwanachama anaweza kuweka akiba yaani saving na kwa ajili ya kutimiza malengo ya mtoto (Elimu) Kwa kuweka fedha kuanzia sh.50,000 na kuendelea.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.