Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti ikiongozwa na Mwenyekiti wake Ramadhani Mpendu aliyeongoza Baraza la Madiwani kupitisha na kujadili taarifa za Hesabu za mwisho za Halmashauri ya Kibiti kwa mwaka wa fedha 2021/2022 lililofanyika tarehe 29/9/22 katika ukumbi wa Halmashauri hiyo .
Katika mkutano huo waheshimiwa Madiwani wamepitisha mchakato wa ufungaji wa ripoti za hesabu za mwisho za Halmashauri hiyo kwa mwaka wa fedha 2021/22 zinazoishia tarehe 30 june 2022 uendelee kwa ajili ya kuwasilisha katika ofisi ya ukaguzi wa Taifa.
Naye Diwani wa kata ya Kibiti Hamidu Ungando katika mkutano huo amesema Halmashauri ya wilaya ya kibiti imeandaa hesabu za mwisho wa mwaka kwa kipindi cha mwaka 2021 /22 na hesabu hizo zimeandaliwa kwa kuzingatia viwango vya kimataifa
Halmashauri ya wilaya ya kibiti ina jumla ya waheshimiwa madiwani 22 ambapo 16 ni wa kuchaguliwa na 06 ni wa kuteuliwa Pamoja na mhe, Mbunge ambaye yuko madarakani kwa kipindi cha miaka 5. Baraza la madiwani limekuwa likikaa vikao vyake mbalimbali vya kawaida kwa kila robo ya mwaka na vikao maalum kwa ajili ya kuamua mambo muhimu yanayohusu uongozi na utawala bora.
Hata hivyo kamati ya ukaguzi ya Halmashauri kupitia vikao vyake vya kila mwaka na vikao maalum vilivyofanyika imekuwa ikishauri kitaalam mambo yote muhimu ya Halmashauri ikiwa ni Pamoja na sheria na kanuni zinazotumika.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.