BARAZA LA MADIWANI HALMASHAURI KIBITI LAPITISHA BAJETI YA BILIONI THELATHINI NUKTA NNE
Halmashauri ya Kibiti Mkoa wa Pwani kupitia baraza lake la Madiwani limepitisha makisio ya Bajeti ya mwaka wa fedha 2021/2022 kiasi cha shilingi bilioni 30.4 ikiwa ni ongezeko la kiasi cha shilingi bilioni 9 ikilinganishwa na bajeti ya mwaka wa fedha 2020/2021 ongezeko hili kubwa linatokana na makisio ya mishahara.Makisio haya ya bajeti kuna fedha za Mishahara,Ruzuku ya kawaida,matumizi mengineyo,Fedha za ruzuku ya miradi ya maendeleo na Fedha za mapato ya ndani(Own source proper) ambayo ni Tsh.1,831,441,270.00.
Aidha,Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Kibiti Ndg.Mohamed I. Mavura alieleza kipaumbele cha Halmashauri katika mwaka wa fedha 2021/2022 ni uboreshaji wa miundombinu ya elimu.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.