Baraza la Madiwani katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti ya Wilaya ya Kibiti limepitisha rasimu ya mpango na bajeti kwa mwaka wa fedha 2025/2026 katika mkutano wa Baraza la Wah.Madiwani la robo ya pili kwa mwaka wa fedha 2024/2025.
Akizungumza wakati wa Baraza hilo kwa niaba ya Waheshimiwa Madiwani Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti Mhe.Ramadhani Mpendu amesema wameridhia kwa pamoja upitishwaji wa bajeti hiyo iliyowasilishwa katika baraza hilo na Mkuu wa Idara ya Mipango Ponsian Kazee.
Katika hatua nyingine Baraza hilo limefanya mchakato wa kumpata makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti ambapo Mhe.Zalia A.Minguya alipata uungwaji mkono wa Waheshimiwa madiwani kwa ajili ya kushika nafasi hiyo.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.