Agosti 14, 2024 Baraza la Maendeleo ya kata Wilayani Kibiti limepokea taarifa za Maendeleo ya kata 16 za Wilaya hiyo kwa robo ya 4 ya mwaka wa fedha 2023/2024 katika ukumbi wa Halmshauri likiongozwa na Kaimu Mwenyekiti Mhe.Omary Twanga.
Mara baada ya kupokea taarifa hizo Waheshimiwa Madiwani walisema, Kutokana na upungufu wa watendaji Kata katika maeneo ya Delta wanaomba Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Ndg Hemed Magaro kuangalia suala hilo kwa ukaribu ili kuweka msawazo wa utendaji kazi katika maeneo hayo.
Mbali na hilo pia Madiwani hao wamemwagiza Mkurugenzi Magaro kuunda timu ya kutambua idadi ya walimu wa kike waliopo Wilayani na kuhakikisha kunakuwepo na walimu wa kike katika kila shule jambo litakalosaidia wanafunzi wa kike kupata huduma katika shule zote.
Katika kikao hicho Kaimu Mkurugenzi Ndg. Denis Kitali Alisema, maoni, maelekezo na mapendekezo yoye yaliyotolewa ameyapokea huku akiahidi kuyafanyia kazi.
Mwisho Kaimu Mwenyekiti wa kikao Mhe. Omary Twanga aliwashukuru wajumbe kwa usikivu waliounyesha na kupokea taarifa za maendeleo ya Kata zote.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.