16.04.2024
Meneja wa Mawasiliano na Mahusiano ya Umma Ndg. Bhoke Rioba wa Kampuni ya mafuta ya Camel ya jijini Dar es Salaam inayosambaza na kuuza kwa wingi mafuta ya bulk ndani na nje ya nchi amemkabidhi msaada wa magodoro 100 na sukari kg 300 Mkurugenzi Mtendaji wa wa Halmashauri ya Kibiti ikiwa ni sehemu ya kurejesha upendo kwa wananchi wa Kibiti waliokumbwa na Mafuriko na kupata hasara kubwa.
Akikabidhi msaada huo kwa Ndg. Ryioba amesema msaada huo ni sehemu ya utamaduni wa Kampuni yao kurejesha upendo kwa wananchi wanaofikwa na madhira mbalimbali hivyo wameamua kuja Kibiti kutoa pole.
"Tumekuwa tukiguswa na matukio ya watanzania wenzetu, poleni sana Kwa janga hili, Kwa niaba ya Kampuni tunaomba mpokee upendo wetu, tumepata hiki, tukaona tuwakimbilie, tuko pamoja nanyi katika kipindi hiki kigumu" Alisema Rioba.
Akipokea msaada huo Mkurugenzi Mtendaji Ndg. Hemed Magaro ameishukuru Kampuni ya Camel kufika kuwafariji huku akibainisha kwamba msaada waliowapatia ni muhimu sana kwani ni moja ya uhitaji mkubwa kwa sasa.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.