25.04.2024.
Shirika la CARITAS linalojishughulisha na kutoa misaada na kuleta maendeleo kwenye jamii chini ya kanisa katoliki pamoja na Rapid wamewasili wilayani Kibiti kutoa misaada mbalimbali pamoja na kufika kujionea hali halisi ya Mafuriko wilayani humo.
Akitoa pole kwa Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Fr. Chescko Msaga kutoka Baraza la maaskofu katoliki TEC amesema katika kutimiza wajibu wao, wamefika na vifaa mbalimbali ambapo wamekabidhi magodoro 150, mablanketi 120, neti 100, shuka 120, nguo mchanganyoko pamoja na viatu boksi 1 kwaajili ya watoto wa jinsia zote na watu Wazima pia.
Akipokea msaada huo Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Kanali Joseph Kolombo amewashukuru kwa misaada hiyo muhimu kwa wahitaji na akawaombea baraka zaidi pale walipotoa.
Kwa niaba ya Mkoa wa Pwani Afisa Tawala Msaidizi mipango na uratibu Bi. Edina Katalaiya amelishukuru shirika hilo kwa kuwajali waathirika wa mafuriko Kibiti, pia amesema misaada hiyo imefika wakati muafaka kutokana na mahitaji, japo namna ya kuwafikia walengwa ni ngumu na njia iliyobaki ni ya usafiri wa majini pekee.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.