Msimamizi wa Uchaguzi jimbo la Kibiti Ndg. Hemed S. Magaro amwemtangaza Bw. Athumani Ally Mketo aliyekuwa Mgombea wa Udiwani Kata ya Mlanzi kupitia Chama Cha Mapinduzi kuwa ndiye Mshindi wa Udiwani Kata hiyo.
Akitangaza matokeo hayo Bw. Magaro alisema, Wapiga kura waliojiandikisha walikuwa ni 4,370. Idadi halisi ya waliojitokeza kupiga kura ni 1,744. Kura halali zilizopigwa ni 1,732 na kura zilizoharibika ni 12. Jumla ya wagombea 8 walijitokeza kugombea nafasi ya Udiwani katika Kata ya Mlanzi ambapo matokeo yalikuwa kama ifuatavyo:
Bw. Hamisi Ngatakwa wa UMD alipata kura 1, Bw. Juma Maramuah wa UDP alipata kura 3, Bw. Said Bambo wa Demokrasia Makini alipata kura 3, Bw. Mzuzuri Sadick wa NRA alipata kura 9, Bw. Amiri Mwambasafu wa ACT Wazalendo alipata kura 15, Bw. Yusuphu Mbolembole wa UPDP alipata kura 18, Bw.Hamis Makitia Abdallah wa CUF alipata kura 91 na Bw. Athumani Ally Mketo wa CCM alipata kura 1,592. Hivyo basi Bw. Mketo ameshinda kwenye uchaguzi huo kwa asilimia 91.9 ya kura halali zilizopigwa.
Baada ya kutangaza matokeo hayo Msimamizi wa Uchaguzi alimkabidhi cheti cha Ushindi Bw. Mketo papohapo. Nao wagombea na wawakilishi wa Vyama vyote vya upinzani vilivyoshiriki walisema wameridhishwa na mwenendo wa Uchaguzi huo kwani ulikuwa wa huru na haki. Wameyapokea matokeo na kumpongeza mshindi.
Uchaguzi huo umefanyika jana Jumatano, tarehe 20 Machi, 2024.
Hongera sana Mh. Athumani Ally mketo kwa kuchaguliwa kwa Kishindo kuwa Diwani wa Kata ya Mlanzi, Kazi iendeleee….
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.