CHANJO YA UVIKO-19 YAZINDULIWA KIBITI.
Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Kanali. Ahmed Abasi Ahmed leo tarehe 03.08.2021 amezindua chanjo ya UVIKO-19 ambayo ni mahsusi kwa ajili ya kujikinga na ugonjwa wa CORONA.
Zoezi hili lilifanyika kwenye kituo cha afya Kibiti,Katika Wilaya ya Kibiti chanjo hii itatolewa kwenye vituo vinne(4) ambavyo ni kituo cha Afya Kibiti,Zahanati ya Bungu,Zahanati ya Jaribu Mpakani,Zahanati ya Nyamisati na Mchukwi Mission Hospitali.
Zoezi hili limeanza kwa makundi tofauti yaliyopewa kipaumbele ambayo ni wahudumu wa Afya,Wazee na watu wenye magonjwa sugu.
Aidha, mheshimiwa mkuu wa Wilaya aliwaomba Wananchi kujitokeza kwa wingi ili kufanikisha zoezi hili muhimu.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.