Wakati Wanafunzi wa Darasa la Saba nchini wakijiandaa kufanya Mtihani wa Taifa Septemba 11 na 12, 2024 Afisa Elimu Divisheni ya Awali na Msingi wilayani Kibiti Mwl. Zakayo Mlenduka amewataka Wazazi, Walezi na Walimu pia kuwasihi watoto wao kufanya mitihani hiyo kwa ufasaha ili waweze kufaulu vizuri.
Afisa huyo amesema katika Wilaya ya Kibiti kuna jumla ya Watahiniwa 4344 ambapo Wavulana ni 1881 na Wasichana ni 2463.
Mlenduka alifafanua kuwa kati idadi hiyo Watahiniwa 3 wa kiume ni wenye uoni hafifu ambapo 1 anatoka Shule ya Msingi Kiongoroni na 2 wanatoka katika Shule ya Msingi Rungungu, lakini pamoja na changamoto walizonazo wanafunzi wote wameandaliwa vyema na wapo tayari kufanya mitihani hiyo wakiwa na uhakika na ufaulu mzuri.
Katika pitapita kujionea hali halisi ya maandalizi mashuleni wanafunzi wamesema wamejiandaa vema kufanya mtihani huo na wanatarajia kufanya vizuri.
Kwa habari picha ni Wanafunzi Watahiniwa kutoka katika Shule za Msingi Nyamakonge, Kitundu na Kibiti, wakiwa wenye furaha na wako tayari kuikabili mitihani hiyo.
Baraza la Wahe. Madiwani, Timu ya Menejimenti na Watumishi wote wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti Tunawatakia Heri Wanafunzi wote wa Darasa la 7 katika mitihani yao ya Taifa.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.