KUTOKANA NA UKAKAMAVU WAKE WA KUKIMBIA BILA KUCHOKA
MKUU wa Wilaya ya Kibiti Kanali Joseph Kolombo, amekuwa gumzo kwa wakimbiza Mwenge Taifa, kutokana na UKAKAMAVU aliouonyesha kwa kukimbia sambamba na wakimbiza Mwenge wa uhuru bila kuchoka licha ya umri mkubwa alionao.
Kanali Kolombo ambaye aliteuliwa na Rais Januari 30.2023, kuwa Mkuu wa Wilaya ya kibiti amekuwa DC wa kipekee kwa maeneo yote ambapo Mwenge wa Uhuru 2023 umekwishapita hadi 22/Mei/ 2023. Uhodari na Ushupavu wake katika Mbio uliotia fora umethibitisha maneno yaliyochagizwa na kikundi cha Hamasa Wilayani Kibiti kuwa Kanali Kolombo ni NUSU CHUMA NUSU MTU.
" Tangu tuanze kukimbiza Mwenge wa Uhuru mwezi April, umekuwa DC wa kipekee Mkakamavu mwenye uwezo wa kumudu hekaheka za Mwenge Pamoja na kukimbia muda mrefu bila kuchoka ukiachilia mbali umri wako. Amekimbia Mwanzo mwisho na asubuhi amekimbiza Mwenge mpaka ulipopakiwa kwenye Gari na sina uhakika kama “Record” yako itavunjwa hakika wewe ni Nusu chuma nusu mtu" Alisema Atupokile Elia Mhalila Mkimbiza Mwenge wa Uhuru kitaifa.
Kanali Kolombo amepata sifa hizo lukuki baada kuonekana akikimbia sambamba na wakimbiza Mwenge wa uhuru bila kuchoka wala kupumzika pale Chombo (Mwenge) kilipohitajika kukimbizwa kwa mguu bila kutumia vyombo vya usafiri.
Hayo yamebainishwa na Wakimbiza Mwenge Taifa kwa nyakati tofauti katika salamu za shukrani kabla ya kuelekea Wilaya ya Mkuranga Wakiongozwa na Kiongozi wa mbio za Mwenge Taifa Ndg, Abdallah Shaib Kaim .
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.