Ikiwa ni siku ya pili tangu kuwasili Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Kanali Joseph Kolombo kwa mara ya kwanza amezungumza na wafanyakazi wa idara zote wa Wilaya ya Kibiti baada ya kuteuliwa na Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dr. Samia Suluhu Hassan.
Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Halimashauri ya Wilaya ya Kibiti Ndg, Mohamed Mavura akimkaribisha Mkuu wa Wilaya ameahidi kumpa ushirikiano wa kutosha sambamba na kusoma taarifa ya utendaji ya Wilaya ya Kibiti iliyojitosheleza ikibainisha mafanikio, na changamoto zilizopo ndani ya wilaya katika idara zote.
Akiwa katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo Kanali Kolombo amemshukuru Mhe. Rais Kwa kumteua, zaidi ameomba kupewa ushirukiano wa kiutendaji Ili kuweza kuwatumikia wananchi wa kibiti huku akisema lengo la kukutana ni kujitambulisha Kwa watumishi wa kada zote.
“Nipo hapa kujitambulisha kwenu, ninaomba ushirikiano wa dhati kama mlivyokuwa mkishirikiana na Mhe. Gowele”alisema Kolombo.
Mara baada ya kusikiliza taarifa ya utendaji wa Halmashauri ya Kibiti Kwa upande wa elimu ambako Hali ya ufaulu ni mbaya ameagiza wanafunzi ambao hawajaripoti shule wasakwe na kufika shuleni haraka iwezekenavyo huku akiagiza Wazazi wote ambao ni chanzo Cha watoto kutofika shule waripotiwe haraka, na ameahidi kuendeleza juhudi za kuwaelimisha Wazazi umuhimu wa elimu.
“Serikali ya awamu ya 6 imejitahidi kuwapunguzia mwendo watoto kwa kujenga shule karibu, na elimu inatolewa bila malipo ,kwa nini watoto wasisome”alisema Kanali Kolombo.
“Elimu ni suala la Kitaifa nawapongeza kwa mikakati mliyokwisha iweka nawasisitiza tuhakikishe tunaitekeleza Ili tuweze kufikia lengo la Serikali” Alisema Kolombo.
Mwisho Kanali Kolombo ameahidi kushirikiana na mamlaka husika katika kushughulikia kero zote za migogoro ya ardhi Pamoja na migogoro ya wakulima na wafugaji.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.