KURUGENZI FC YATOKA KIDEDEA KWA KUFUNGA BAO 1-0.
Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Kanali Joseph Kolombo na Mgeni rasmi wa sherehe za Muungano Wilayani Kibiti ashuhudia bonanza la kumbukizi ya miaka 59 ya Muungano 2023 akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali wameadhimisha sherehe za Muungano kwa kushuhudia michezo mbalibali katika uwanja wa Samora.
Katika mtanange huo timu ya Kurugenzi FC Mbele ya Mwajiri wao ndg, Mohamed Mavura, iliibuka kidedea na kujipatia bao la ushindi dhidi ya wapinzani wao wa timu ya Microfinance Traders FC kwa kuitandika bao 1-0.
Katika mechi hiyo bao la ushindi lilifungwa na mchezaji nambari 7 mgongoni Omari Mucky na kuwatuliza Microfince traders mnamo dk ya 8 mara tu baada ya mchezo kuanza. Mpaka mpira unamalizika wapinzani hawakuweza kufurukuta na kuifanya Kurugenzi FC kujinyakulia ushindi huo.
Vilevile kulikuwa na mchezo wa kuvuta kamba kwa wanaume na wanawake kati ya timu hizo, ambapo kwa upande wa wanaume Microfinance ilifanikiwa kuizidi nguvu Kurugenzi FC na kwa upande wa wanawake kurugezi FC ikawa mshindi katika shindano hilo.
Licha ya michezo hiyo pia, kulikuwa na mashindano ya kukimbiza kuku ambapo kwa upande wa wanaume Shabani Mchengo aliibuka mshindi huku kwa upande wa wanawake Aziza Mpeli ndiye aliyeshinda na kila mmoja akapata zawadi ya sh. 10,000.
Hata hivyo mashindano hayo yalinogeshwa na zoezi la kukuna nazi kati ya Sakina Njoro na Omari Mbonde mkazi wa kitembo na wote kutoka droo na kujinyakulia sh. 10,000 kila mmoja.
Awali katika majira ya asubuhi Viongozi, Watumishi, Taasisi, Wanafunzi na Wananchi walishiriki zoezi la kupanda miti katika eneo linalozunguka bwawa la Lumiozi ikiwa ni sehemu ya kuendelea kulinda na kuhifadhi vyanzo vya maji vilivyopo.
Kwa mwaka 2022/2023 wilaya ya Kibiti imefanikiwa kupanda jumla ya miche 1,101,216 ya miti katika maeneo mbalimbali ndani ya Wilaya. Kaulimbiu ya upandaji miti mwaka huu imebeba ujumbe usemao, “Mazingira yangu,Nchi yangu, Naipenda daima”.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.