Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Kanali Kolombo mapema hii leo tarehe 23,Novemba,2024 ameongoza mazoezi ya Pamoja yenye lengo la kuhamasiha wananchi wa Wilaya ya Kibiti kujitokeza kwa wingi kushiriki kupiga kura katika uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika tarehe 27,Novemba 2024.
‘’Niwaombe tujitokeze Kwenda kupiga kura tarehe 27,Novemba ili kuwapata viongozi bora watakaoweza kuongoza kwa maslahi ya Umma na kuweza kusimamia maendeleo katika maeneo yetu’’
Aiha Kanali Kolombo ameongeza kwa kusema kwamba hali ya Usalama katika Wilaya ya Kibiti ni shwari kabisa hivyo wananchi wasiwe na hofu yoyote na viongozi wanaogombea nafasi mbalimbali waendelee kujinadi kama ilivyokusudiwa katika ratiba ya uchaguzi.
Katika hatua nyingine Afisa Uchaguzi wa Wilaya ya Kibiti Bi.Raya Mlawa amewaasa wanakibiti kujitokeza siku ya kupiga kura kwani siku hiyo itakuwa ni maalumu kwa ajili ya zoezi hilo tu.
‘’Kila mmoja ambae amejiandikisha anatakiwa kujitokeza siku ya kupiga kura kwani siku hiyo itakuwa ni ya mapumziko kwa ajili ya kupiga kura’’
Sambamba na hilo Bi.Raya Mlawa amewakumbusha wananchi wa Kibiti vitu maalumu vya kuzingatia pindi wanapoenda kwenye vituo vyao vya kupigia kura ikiwemo kuwa na kitambulisho husika ambacho kitamuwezesha mkazi kupiga kura.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.