Mkuu wa wilaya ya Kibiti Kanali Joseph Kolombo amefanya ziara ya kikazi kukagua eneo la ujenzi wa chuo cha ufundi (VETA) katika kijiji cha Nyambili unaotarajiwa kuanza hivi karibuni ikiwa ni sehemu ya kuongeza wingo wa kitaaluma katika ngazi ya wilaya kwa watoto ambao hawakupata nafasi ya kwenda elimu juu kujiendeleza.
Awali Mtendaji wa Kijiji cha Nyambili Elia Clemence akimkaribisha mkuu wa Wilaya amesema eneo hilo lilitengwa na Serikali ya Kijiji ni salama, lina jumla ya hekta 267ambapo kati ya hizo heka 50 zimetengwa maalum kwa ajili ya ujenzi wa chou hicho.
Kanali Kolombo amesema lengo la ziara yake ni kufika na kujiridhisha juu ya uwepo wa eneo hilo
Aidha, Kanali Kolombo ameagiza Kijiji kuandika muhtasari utakaoainisha maeneo yaliyowazi ili kutambua akiba iliyopo kwa ajili ya shughuli nyingine za maendeleo. Sambamba na hayo amewaagiza Wataalam wa ardhi kupima eneo na kuhakikisha upatikanaji wa Hati Pia amewataka wakuu wa Taasisi za TARURA,TANESCO na Idara ya maji kupima na kuweka miundombinu muhimu ikiwa ni pamoja na barabara, umeme na maji.
Katika hatua nyingine Mkuu wa Wilaya Mhe. Kolombo ametembelea shule mpya ya sekondari Nyambili Nyambunda na kuagiza kuendeleza zoezi la kutoa elimu kwa jamii kuona umuhimu wa watoto kuripoti shule na kuchangia Jumla ya sh 130,000 kwa ajili ya chakula shuleni.
Wakiwa shuleni hapo, Mohamed Mavura ametoa rai kwa wazazi na jamii kwa ujumla katika msimu huu wa kilimo kuhakikisha wanalima mazao ya vyakula jambo litakalorahisisha uchangiaji wa chakula shuleni bila kutumia gharama kubwa.
Kwa mujibu wa Mwalimu wa chakula shuleni hapo amesema katika shule hiyo wameshaanza kulima mbogamboga, migomba, mihogo sambamba na zoezi la kupanda miti ambapo mpaka sasa jumla ya miti 700 kati ya 1400 imeshapandwa.
Vile vile, Kanali Kolombo amekagua kituo cha Polisi Jaribu mpakani ambacho kipo katika hatua ya umaliziaji na kituo cha Polisi bungu ambacho kipo katika hatua ya upandishaji ukuta na kuchangia sh 200,000 Kwa ajili ya kuendeleza ujenzi huo na kusisitiza ujenzi huo kukamilika kwa wakati.
Hata hiyo Mhe. Kolombo amekagua ujenzi wa barabara ya mzunguko ya stendi ya wilaya ya Kibiti inayojengwa kwa kiwango cha lami na kumtaka mkandarasi kuripoti ofisini kwake katika siku ya ijumaa(kesho) tar 10/02/2023 ili kuweka makubaliano ya ni lini ujenzi unakamilika ukizingatia mkataba wake upo ukingoni kumalizika na kazi bado haijaisha.
.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.