Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Kanali Joseph Kolombo amekabidhi hundi ya sh 25,500,000 kwa vikundi 5 vilivyokidhi vigezo ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kutaka kuhakikisha anapunguza umasikini katika jamii na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.
" Ninamshukuru Mhe. Rais kwa kutoa mkopo huu, ndg zangu tumieni fursa hii kuhamasishana kuchukua fedha ili muweze kujiendeleza kiuchumi" Alisema.
Hata hivyo Kanali Kolombo ameiagiza pia Idara ya maendeleo ya jamii kuwafikisha mahakamani Wanavikundi ambao hawatafanya marejesho kwani masharti ya mkopo huo ni pamoja na kurejesha.
Kwaupande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti Mhe. Ramadhan Mpendu amewasihi wananchi kuhakikisha wanafanya marejesho ili fedha hizo zikaweze kukopeshwa vikundi vingine ambavyo havijabahatika kupata katika awamu hii.
Awali Afisa Mikopo wa Wilaya Bi. Sarah Ndumula amesema katika robo hii Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti imetenga jumla ya kiasi cha fedha cha sh 466,221,556.52 ambapo tayari wamepokea maombi 24 yenye thamani ya sh . 312,678,000.
Licha ya hayo pia amesema vikundi 5 kati ya 9 vilivyokidhi vigezo vilihakikiwa vikiwa na maombi yenye thamani ya sh 123, 320,000.00 ambapo mpaka sasa Halmashauri imetenga jumla ya sh 281,927,225.48.kwa ajili ya mikopo hiyo.
Mwisho Bi. Sarah amesema ili kupata mkopo kikundi kinapaswa kusajiliwa kwenye mfumo kielekroniki wa wezesha portal na mpaka sasa wamekwishafanya usajili wa vikundi 113, vikundi 66 vimekamilisha usajili, 22 viko katika mchakato wa usajili, 25 havikukidhi vigezo ambapo vimeelekezwa kufuata taratibu.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.