Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Meja Edward Gowele akiyekuwa akikaimu Wilaya ya Kibiti amekabidhi ofisi rasmi kwa mkuu wa Wilaya ya Kibiti Kanali Joseph Kolombo ambaye ameteuliwa January 25 mwaka huu na Mhe. Rais wa Jamuhuri ya Tanzania Dr Samia Suluhu Hassan.
Akikabidhi ofisi na kuitambulisha kamati ya ulinzi na usalama Meja Gowele ameitaka kamati hiyo kumpa ushirikiano Kanali Kolombo kama walivyokuwa wakishirikiana naye kuhakikisha kibiti inasonga mbele katika kuwatumikia wananchi.
“ninaomba mumpe ushirikiano Kanali Kolombo kama mlivyokuwa mkishirikiana nami tuweze kufikia malengo ya kuwatumikia watanzania , Mhe. Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Kanali Kolombo Kamati hii ya ulinzi na usalama na Mkurugenzi Mtendaji ninawaami Sana”alisema Meja Gowele.
Vilevile Meja Gowele amemkabithi Kanali kolombo ripoti yenye taarifa ya utendaji wa Wilaya ya Kibiti sambamba na kuainisha maeneo yenye migogoro ya ardhi na mipaka ambayo yamekuwa ni changamoto katika Wilaya ya kibiti.
Aidha Mkuu mpya wa Wilaya ya Kibiti Kanali Joseph Kolombo amemshukuru Meja Gowele Kwa kumwonesha ushirikiano tangu siku alipoteuliwa, huku akiomba ushirikiano kwa kamati ya ulinzi na usalama akisema bila wao peke yake hatoweza pia ameahidi kushirikiana nao katika kuhakikisha Wilaya inasonga mbele.
“Peke yangu siwezi bila kupata kushirikiana nanyi, ninaomba tushirikiane”alisema Kanali Kolombo.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.