Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani Kimeitunuku Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti hati ya pongezi kwa usimamizi mzuri wa miradi na uanzishwaji wa miradi mipya kwa nguvu za wananchi. Jambo hilo limejiri Tarehe 22 Nov.2023 katika Mkutano wa Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani wa Kusoma taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya Mwaka 2020-2025, kuanzia Machi 2021 hadi Juni 2023.
Katika Mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere uliopo Kibaha Pwani ukiongozwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani Ndugu. Mwinshehe Mlao, Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti iliibuka kidedea kwenye Usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo lakini pia ubunifu wa miradi mipya ya maendeleo ambayo inatekelezwa kwa nguvu za wananchi.
Bw. Mlao amefurahishwa sana na ari na umoja wa wananchi wa kibiti katika kuhakikisha maendeleo yanapatikana kwa nguvu zote. Moja ya miradi hiyo gumzo ni Shule ya Sekondari ya Wananchi inayojengwa katika kata ya Kibiti kwa nguvu za wananchi wenyewe ambayo kwasasa imefikia katika hatua ya kufungwa renta.
Hati hiyo imepokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Kibiti, Kanal Joseph Kolombo ambaye aliongozana na Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti.
Pongezi hizi ni zetu sote WanaKibiti na huu ni mwanzo tuu.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.