22.09.2024.
Wakati tukijiandaa kuelekea katika Uchaguzi wa Serikali za mitaa Novemba 27 mwaka huu na Uchaguzi Mkuu hapo mwakani Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Taifa Ndg. Ally Hapi amesisitiza kuchagua Viongozi makini huku akikipigia debe Chama cha Mapinduzi kupigiwa kura kwa wingi ili kiweze kuendelea kushika dola na kuleta maendeleo nchini.
"Ninapenda kuwakumbusha kukiunga mkono chama Cha Mapinduzi katika chaguzi za serikali za mitaa, vijiji na vitongoji, pamoja na uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwakani”.
Hayo yamesemwa Jana septemba 22, 2024 na Katibu huyo wa Jumuiya ya Wazazi Taifa Mhe. Ally Hapi alipokuwa katika katika ziara ya kikazi Wilayani humo.
Ndg. Hapi amewataka wanaccm na wananchi kwa ujumla kuchagua wagombea wenye sifa wanaokubalika kuchukua fomu za ugombea ikiwa ni pamoja na kuhakiki ama kujiandikisha kwenye daftari la wakazi litakalotoa sifa ya utambuzi wa kugombea na daftari la kudumu la kupiga litakalotoa sifa ya kupiga kura wakati wa zoezi hilo utakapofika.
Hata hivyo Hapi amewataka Viongozi wa Chama hicho kujipanga vizuri na kuimarisha umoja na mshikamano ili kuhakikisha Kibiti inasonga mbele kimaendeleo na kupata ushindi wa kishindo katika chaguzi zote zijazo.
Aidha katika chaguzi hizo zijazo Hapi amesisitiza na kuwataka wanachama na wananchi pia kuwa makini kwa kuepukana na tabia za ugombanishi, uchochezi na kufitinishwa na makundi ya watu wachache wasio waadilifu ambao kwa namna moja ama nyingine huweza kuwaharibia amani iliyopo.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.