MWENGE wa uhuru umepokelewa Mkoani Pwani, kutoka Mkoa wa Morogoro ambapo ukiwa Mkoani hapo utapitia Miradi 99 yenye thamani ya trilioni 4.4.
Akipokea Mwenge huo, eneo la Ubena Estate Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Alhaj Abubakari Kunenge, anaeleza kati ya miradi hiyo miradi 55 itakaguliwa, 9 itafunguliwa, 15 itazinduliwa na 20 itawekwa mawe ya msingi.
"Miradi hiyo inadhihirisha kazi nzuri inayofanywa na Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan "
Aidha Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Col. Joseph Kolombo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti Mhe. Ramadhan Mpendu, kaimu Mkurugenzi Mtendaji Ndg. Denis Kitali Pamoja na badhi ya Wakuu wa Idara na Vitengo walifika hadi Chalinze katika eneo la Ubena Estate kushuhudia mapokezi hayo ya mwenge Mkoani Pwani.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.