Mkuu wa masoko na mambo ya kijamii Jenga Tanzania Agriculture ambao ni wawekezaji wapya wa kilimo cha Alizeti Wilayani Kibiti Bi. Amilia Basil ametembelea Banda la nanenane Wilaya ya Kibiti katika Viwanja vya Mwl Nyerere Manispaa ya Morogoro.
Bi.Amilia amesema, amefurahishwa na kuridhishwa na bidhaa zilizopelekwa kwenye maonyesho hayo kutokana na uhalisia wa malighafi zinazopatikana kibiti.
"Kwa kuwa na Mimi ni mjasiriamali nitawaunga mkono kinamama hawa kwa kuchukua sabuni za mchezo wanazotengeneza kwa jumla" Alisema Bi. Amilia.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.