Msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Kibiti Ndg. Hemed S. Magaro amewaapisha Makarani waongozaji wa Wapiga kura kwaajili ya Uchaguzi mdogo wa udiwani katani Mlanzi kwa mujibu wa sheria na sehemu ya maandalizi ya uchaguzi huo utakaofanyika tarehe 20.03.2024
Makarani hao wamekula kiapo cha kutunza siri pamoja na kutoa tamko la kujitoa au kutokuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa kama sheria inavyowataka.
Pia Makarani wamepata mafunzo ya kujengewa uwezo wa namna wanavyopaswa kuifanya kazi hiyo kwa nadharia na Vitendo.
Yote hayo yamejiri Leo tarehe 16.03.2024.
Pichani ni badhi ya matukio hayo.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.