Jumla ya Tani 20,150 zenye thamani ya sh. Mil 65 zimeuzwa katika msimu wa korosho Mkoa wa Pwani huku hali ya bei ya korosho ikiridhisha na kuwapelekea matumaini wakulima ambapo waliweza kuuza kwa bei ya wastani wa juu kwa sh .4000 na wastani wa chini kuuzwa kwa sh 3800.
Hayo yameelewa na Hamis Mantawela Meneja wa Corecu Mkoa wa Pwani katika mnada wa 8 na wa mwisho msimu huu uliofanyika katika viunga vya Corecu Wilayani Kibiti.
Mantawela amesema licha ya kuwa na msimu mzuri na bora kuwahi kutokea Mkoa wa Pwani walipitia changamoto ya uhaba wa maghala uliopelekea kutafuta maghala shikizi kutokana na wingi wa korosho kwenye ghala kuu.
Katika kutekeleza agizo la Serikali kuhakikisha malipo ya wakulima yanalipwa kutoka chama kikuu, Mantawela amesema wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutekeleza kwa kushirikiana na mabenki kuhakikisha malipo yanatoka kwa wakati .
Aidha Meneja Mantawela amewasihi wakulima wote kuhakikisha taarifa za kibenki kwa kila mkulima zinakuwa sahihi ili kuepuka changamoto zinazojitokeza na kusababisha kuchelewa kwa malipo.
Kwa upande wa uzalishaji wa zao hilo Wakulima wameshauriwa kuendelea kuzalisha kwa wingi na kudhibiti ubora wa korosho zao ili kuweza kupata masoko ya uhakika bila kusuasua.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.