Mkuu wa Wilaya ya Kibiti, Kanali Joseph Kolombo ameongoza kikao cha kamati ya Afya ya msingi ngazi ya Wilaya ya Kibiti, kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti siku ya Alhamisi Tarehe 14.12.2023
Mada kubwa iliyojadiliwa katika kikao hicho ni Mradi wa WASH (PforR). Alipokuwa akielezea kuhusu mradi huo Bw. Laban Kitule ambaye ni Afisa Afya na mwezeshaji wa kikao juu ya mradi huo alisema;
“Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti ni miongoni mwa Wilaya 8 katika mkoa wa Pwani zinazotekeleza mradi wa WASH(PforR) kwa mwaka wa fedha 2023/2024”.
Bw. Kitule alieleza kuwa Wilaya ya Kibiti imepokea kiasi cha fedha Jumla ya Tsh. 238,848,519.12 kama mbegu kwaajili ya utekelezaji wa ujenzi wa miundombinu ya vyoo katika vituo 5 vya kutolea huduma za Afya ambavyo ni zahanati 4 na Kituo cha Afya 1.
Vituo hivyo ni: Zahanati ya Ruaruke, Zahanati ya Rungungu, Zahanati ya Bungu, Zahanati ya Mchukwi pamoja na kituo cha Afya Kibiti.
Bw. Kitule aliendelea kueleza kuwa lengo la mradi huo ni:
Mpaka sasa shughuli ambazo zimeshatekelezwa ni kuhamasisha ujenzi wa vyoo bora ngazi ya kaya na Kujenga miundombinu ya usafi wa mazingira katika Zahanati na Kituo cha Afya.
Aidha kwa kutekeleza vyema mradi huu Halmashauri, Vituo na Kaya zote zitanufaika kama ifuatavyo:
Akichangia kikao hicho Kanali Kolombo ameishukuru serikali ya Awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa jitihada kubwa za kuleta maendeleo nchini lakini pia kujali Afya za Wananchi wake kwa kutuletea miradi kama hii.
Kanali Kolombo aliongeza kuwa mradi huu ni muhimu hivyo unahitaji uhamasishaji na uelimishaji wa kutosha kwa wananchi ili uweze kutekelezwa na kuleta tija kama ilivyokusudiwa.
Akieleza juu ya mikakati iliyopo Mganga Mkuu wa Wilaya Dkt. Elizabeth Oming’o amesema Idara ya Afya tayari imeshachukua hatua ya Kuelimisha Umma juu ya umuhimu wa choo bora kupitia Maafisa Afya waliopo pamoja na wenyeviti wa vijiji kwa maeneo yatakayopitiwa kama mfano wakati wa ukaguzi.
Maeneo hayo ni Kata ya Bungu pamoja na Kibiti hivyo anawasisitiza Wananchi wote hususani wa maeneo tajwa kudumisha usafi sio wa vyoo tuu bali ni pamoja na mazingira yanayowazunguka.
Naye Diwani wa Kata ya Kibiti Mh. Hamidu Ungando alisema, mradi huu ni muhimu sana sio kwasababu utawapatia kaya husika fedha lakini utaepusha magonjwa ya mlipuko ambayo serikali hutumia gharama nyingi sana kukabiliana nayo badala ya kutumia fedha hizo kuleta maendeleo.
Akimalizia kuchangia kikao hicho Sheikh Thabit Milindo wa Wilaya ya Kibiti alisema usafi ni muhimu mno hata vitabu vya dini vinasisitiza hilo, ndiyo maana hata mahali wakitaka kujenga Msikiti wanaanza kujenga kwanza choo.
Kanali Kolombo ametoa rai kwa Wananchi wote wa Wilaya ya Kibiti kuhakikisha kuwa kila kaya inakuwa na choo bora lakini pia wafanye matumizi sahihi ya vyoo hivyo.
“Hakutakuwa na maana ikiwa watu wamejenga vyoo bora lakini bado wanajisaidia vichakani, msijenge vyoo kama mapambo, jengeni na mvitumie ili kuweka safi mazingira yetu” Alisema Kolombo
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.