Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango imetembelea Miradi ya Maendeleo mwaka wa Fedha 2024/2025 ambapo imefanya ukaguzi wa Miradi mbalimbali ikiwemo Ujenzi wa vyoo, Shule Mpya ya Sekondari katika kata ya Mbuchi, Mradi wa Mifumo ya maji,kinawia mikono,shimo la kutupia Kondo la Nyuma,Shimo la Kutupia Majivu,Kichomea Taka na Matundu ya Vyoo Zahanati ya Nyambili.
Aidha Miradi mingine iliyotembelewa na Kamati hiyo ni Ujenzi wa vyumba Vinne vya Madarasa na Matundu Sita ya vyoo katika Shule ya Msingi Kibiti(BOOST) na Ujenzi wa Shule Moja ya Awali katika Shule ya Msingi Nyamakonge, pamoja na Vikundi Vitatu vinavyojumuisha Kikundi cha Wanawak(Amani Wamama Mgaru kinachojishughulisha na Kilimo cha Ufuta,Kikundi cha Wanawake(Jikomboe Group) kinachojihusisha na Biashara ya Mama Lishe na Kikundi cha Vijana Bungu (youg fighter) kinachojihusisha na Biashara ya Genge.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.