KAMATI YA FEDHA UTAWALA NA MIPANGO YATEMBELEA NA KUKAGUA MIRADI MBALIMBALI YA MAENDELEO KWA KIPINDI CHA ROBO YA NNE MWAKA 2021.
Leo tarehe 19/07/2021 wajumbe wa kamati ya Fedha Utawala na Mipango walitembelea na kukagua maendeleo ya ukarabati na ujenzi wa miradi mbalimbali ya sekta ya Afya,Elimu na Utawala.
Miradi iliyotembelewa na kukaguliwa ni ukarabati wa Zahanati ya Mchukwi na ujenzi wa nyumba ya mganga ,ukamilishaji wa ujenzi wa maabara shule ya sekondari Mchukwi, ujenzi wa madarasa mawili,ofisi ya walimu na vyoo matundu 12 shule ya sekondari Zimbwini,ujenzi wa jengo la Halmashauri ya Wilaya,ukamilishaji wa ujenzi wa madarasa shule ya msingi Roja,Ujenzi wa wodi 3 za wanaume,wanawake na watoto hospitali ya Wilaya,ujenzi wa vyumba 2 vya madarasa na ofisi shule ya msingi Msafiri na ukamilishaji wa ujenzi wa maabara shule ya sekondari Mahege.
Kiasi cha shilingi 1,315,723,771.17 zitatumika mpaka kukamilika kwa miradi hii,chanzo cha fedha hizi ni ruzuku toka serikali kuu,RBF,EP4R na COVID 19-GPE.
Aidha,kamati iliridhishwa na maendeleo ya ujenzi na kuagiza wataalamu kuongeza kasi zaidi kwenye kusimamia miradi ili iishe kwa wakati kwa kuzingatia viwango vinavyohitajika.Picha zaidi bofya hapa
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.