Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti Mhe. Ramadhani Mpendu akiwa ameambatana na Mkurugenzi Mtendaji Ndg. Mohamed I. Mavura pamoja na wakuu wa Idara wa Wilaya ameongoza ziara ya kamati ya fedha mipango na uongozi kukagua miradi ya maendeleo inayoendelea katika Wilaya ya Kibiti kwa mwaka wa fedha 2022 -2023.
Katika ziara hiyo Mwenyekiti Mpendu amepongeza kasi nzuri ya ujenzi ilipofikia katika miradi yote na kuzitaka kamati zote za ujenzi kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati uliokusudiwa.
Kutokana na uhaba wa shule za sekondari za kidato cha 5 na 6 Wilayani hapa, Mkurugenzi Mtendaji Mohamed Mavura ametoa pendekezo shule ya sekondari Dimani kuandaliwa kuwa na kidato cha tano na cha sita jambo ambalo litafanya watoto kuvutiwa na kuendelea kupata huduma hiyo ndani ya Wilaya na wanaofaulu kwa sasa wanalazimika Kwenda nje ya Wilaya yetu, Kwani Wilaya ya Kibiti Kuna sekondari ya wavulana Kibiti pekee ambayo bado haikidhi mahitaji hususani kwa watoto wa kike.
Wakiwa katika shule za sekondari zenye mradi wa 420,000,000 fedha za Serikali Kuu wenye jumla ya vyumba 21 vya madarasa,Kata ya Dimani hali ya ujenzi wa darasa moja lenye thamani ya sh .20,000,000. katika sekondari ya Dimani upo hatua ya upauzi,Kata ya mtawanya sekondari ya mtawanya ujenzi wa vyumba 9 vya madarasa vyenye thamani ya 180,000,000 upo hatua ya upauaji,Kata ya Bungu sekondari ya Nyambili Nyambunda vyumba 5 vya madarasa vyenye thamani ya sh 100,000,000 ujenzi upo hatua ya upauaji sambamba na ujenzi wa choo tundu 13 zenye thamani ya sh 20,000,000 kwa fedha za mapato ya ndani wakati ambao upo Hatua ya msingi na katika sekondari ya Mwambao ni vyumba 6 vya madarasa vyenye thamani 120,000,000 ambapo pia ujenzi upo hatua ya upauaji.
Vilevile kwa upande wa miradi ya shule za msingi, kamati imeitembelea shule ya msingi Roja katika Kata ya Mtawanya ambapo ujenzi wa darasa moja lenye thamani ya sh 20,000,000 umekamilika kwa fedha za mapato ya ndani, Kata ya Bungu shule ya msingi Songas vyumba 2 vya madarasa vyenye thamani ya 43,000,000 ujenzi upo hatua ya umaliziaji kwa ufadhili wa kampuni ya gesi ya Songas.Pia katika Kata ya Kibiti shule ya msingi ujenzi wa vyumba 2 vya madarasa ya awali wenye thamani ya sh.55,824,000 kwa fedha za LANES upo katika hatua ya umaliziaji.
Aidha kamati ulifanikiwa kufika katika hospitali ya Wilaya iliyopo Kata ya Mtawanya, na kujionea hali halisi ya ujenzi wa Jengo la wagonjwa wa dharula (EMD) lenye thamani ya sh 300,000,000 kwa fedha za uviko upo katika hatua za ukamilishaji, ujenzi wa majengo 4 yenye thamani ya sh 800,000,000 kwa fedha za Serikali Kuu, Jengo la kuhifadhia maiti (mortual) ujenzi upo hatua ya umaliziaji, Jengo la upasuaji (theatre) lipo hatua ya upauaji vilevile ujenzi wa wodi 2 za wagonjwa waliofanyiwa upasuaji (surgical ward ) kwa wanawake na wanaume ziko hatua ya upauaji.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.