KAMATI YA FEDHA UTAWALA NA MIPANGO YAFANYA UKAGUZI WA MIRADI ROBO YA PILI.
Kamati ya Fedha Utawala na Mipango leo tarehe 22-02-2021 imefanya ukaguzi wa miradi mbalimbali ikiwemo ya elimu Msingi ,Sekondari pamoja na Utawala.
Miradi iliyotembelewa leo ni shule ya msingi Motomoto ambayo ilipata changamoto ya paa kuezuliwa na upepo na Mkueugenzi mtendaji aliwapa kiasi cha zaidi ya milioni kumi na sita toka mapato yake ya ndani kwa ajili ya ukarabati na teyari ukarabati umefanyika na wanafunzi wanaendelea na masomo,kamati ilitembelea kikundi cha kinamama wajasilia mali kinachoendesha shughuli zake shule ya sekondari Kibiti ambacho kilipatiwa mkopo kiasi cha shilingi milioni nne kwa awamu ya pili ,kikundi kinaendesha mgahawa na kinaendelea vizuri.
Pia kamati ilitembelea jengo la ghorofa mbili la ofisi ya Halmashauri ya Kibiti ambalo ujenzi wake unaendelea kwa sasa lipo kwenye hatua ya ukamilishaji chanzo cha fedha za ujenzi zimetolewa na serikali kuu.
Aidha Mhe mwenyekiti wa Halmashauri pamoja na kamati yake wameridhishwa na usimamizi mzuri wa miradi na kutoa pongezi kwa Mkurugenzi Mtendaji pamoja na watendaji wote na kuahidi kuwapa ushirikiano wa dhati katika kuhakikisha Kibiti inakwenda mbele na kutoa huduma bora kwa wananchi wake.
IMETOLEWA NA KITENGO CHA TEHAMA NA UHUSIANO HALMASHAURI YA KIBITI
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.