Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti Bw. Hemed Magaro amefungua kikao kazi cha kamati ya uratibu wa Maafa ya Wilaya ya Kibiti chenye lengo la kujadili na kuweka mikakati ya kukabiliana na mvua za el -nino zinazotarajiwa kuanza mwezi huu nchini ambazo zinaweza kuweza kusabanisha Maafa katika maeneo ya mabondeni wilayani Kibiti.
" Tumepokea taarifa ya uwezekano wa uwepo wa maafa yatokanayo na mvua za elnino katika mikoa 14 Tanzania ikiwemo na Mkoa wa Pwani." Alisema Hemed Magaro.
Katika kikao hicho Mkurugenzi Hemed Magaro amewataka Wajumbe walioshiriki kikao hicho kuitikia wito mara wanapoitwa kwa ajili ya kutekeleza majukumu yao muda na wakati wowote pindi watakapohitajika katika zoezi la maafa.
" Niwaombe , muwe tayari kuitikia wito wakati wowote mtakapohitajika, nyie ni Kamati ya Wataalam ya maafa, tunategemea maelekezo yenu" Alisema Magaro.
Vilevile Magaro amesema katika kuhakikisha wanakabiliana na janga hilo wameweka mikakati mbalimbali itakayosaidia kutekeleza usimamizi wa maafa ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kupitia njia mbalimbali ili jamii iweze kupata uelewa wa nini kinaweza kutokea na namna ya kujiokoa.
Vilevile amesema mikakati mingine waliyoweka Kwa pamoja wameaximia kuhakikisha kunakuwepo na vifaa vya kutosha vya uokoaji sambamba na rasilimali watu, kuandaa bajeti ya dharura ya maafa, kutoa njia za mawasiliano, kujua idadi ya watu wanaoishi katika maeneo hatarishi n.k
Hata hivyo Magaro ameagiza idara ya afya kuhakikisha kunakuwa na akiba dawa za kutosha hasa kipindi hiki tunachotarajia mvua za el nino kuanza kunyesha. Pia amesisitiza vyombo vya usafiri majini na nchi kavu vikarabatiwe na viwe tayari wakati wowote kuanzia sasa.
Mbali na hayo, Mwenyekiti Magaro ameagiza idara ya kilimo kuandaa mbegu za mazao ya muda mfupi kutumika kupunguza changamoto ya chakula baada ya mafuriko kutokea kwani kitaalamu maeneo yanayopitiwa na mafuriko hustawisha sana chakula katika ukanda wa bonde la mto Rufiji.
Naye Mratibu wa Maafa Wilaya ya Kibiti Bw. Gideon Zakayo amesema katika Wilaya ya Kibiti maeneo ambayo wananchi wanaweza kuathiriwa na mvua za elnino ni katika Kata ya Mtunda maeneo ya Nyambele, Nganyanga, beta, mbwanga na kifimbo, Kata ya maparoni ni maeneo ya usimbe kiwanjani,gingi,mbangani na usimbe kidoga, na Kata ya mbuchi ni maeneo ya kipoka, mikwang'ombe, barabarani na kumbacha wakati katika Kata ya msala ni tarachu na domwe kwani maeneo haya yapo bondeni mwa mto Rufiji hata mvua za mwaka 2020 zilileta athari kwa maeneo hayo..
Aidha Mratibu wa maafa Zakayo amesema katika kipindi hicho maeneo ambayo wananchi wanaweza kuhamia kujisitiri katika Kata ya Mtunda ni Kijiji cha Mtunda A, Kata ya mbuchi maeneo salama ni nganje na kitingi, Kata ya msala ni kisimbya na twasalie wakati huo huo Kata ya Ruaruke na kikale ni yameonekana kuwa maneno salama zaidi katika misimu yote wilayani kibiti.
Katika kikao hicho SGT. Boniface Kijumbe kutoka kikosi cha zimamoto Wilaya ya Mkuranga amesisitiza Taasisi ya Tarura Wilaya ya Kibiti kwa kushirikiana na Maafisa wa Idara ya Afya na Mazingira kuhakikisha taka hazirundikwi au kutupwa hovyo, kuzibua mitaro na kuhakikisha wanatengeneza njia za dharura ili mvua zitakapoanza kunyesha takataka zisizuie maji kupita Kwa urahisi.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.