Tarehe 5.7.2024 Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Kanali Joseph Kolombo amefunga rasmi mafunzo yaliyokuwa yanatolewa kwa Kamati ya Maafa Wilayani Kibiti.
Mafunzo hayo yaliyoendeshwa na Wakufunzi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu kitengo cha Maafa yamedumu kwa siku 5 toka toka Julai 1 hadi 5, 2024 lengo likiwa ni kujifunza namna ya kuzuia, kujiandaa na kukabiliana na maafa mbalimbali pindi yatakapotokea.
Akiwa katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri Kanali Kolombo amewashukuru wakufunzi hao toka Ofisi ya Waziri Mkuu na wadau mbalimbali kwa kuwezesha mafunzo hayo kwakuwa yatakwenda kuwasaidia endapo majanga yatatokea.
Kanali Kolombo amesema kuwa kuzingatia kuwa Wilaya ya Kibiti ni moja ya Wilaya ambazo zimepitiwa na mto Rufiji, bomba la gesi na Barabara kuu ya kilwa basi ipo kwenye hatari ya kukumbwa na lolote wakati wowote, hivyo mafunzo hayo yatawasaidia endapo janga lolote litatokea.Kupitia mafunzo hayo amewasihi washiriki ambao ni Kamati Elekezi na Kamati ya Maafa ya Wataalam kuhakikisha mafunzo hayo yanatekelezwa kwa vitendo endapo janga lolote litatokea katika Wilaya ya Kibiti.
Kwa habari picha ni Kamati Elekezi ya maafa na kamati ya Wataalam wakiwa katika mafunzo kwa nyakati tofauti.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.