Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Kanali Joseph Kolombo akiwa ameambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama pamoja na Wataalam wa Halmashauri ya (W) wamekuwa na ziara ya kutembelea na kukagua miradi inayotarajiwa kumulikwa na Mwenge wa Uhuru 2025 utakaopokelewa mwezi aprili 07 Wilayani Kibiti.
Miradi iiliyotembelewa ni eneo la mapokezi ya mwenge Zimbwini sekondari, mradi wa mazingira na Uraghabishaji shule ya msingi Kibiti, mradi wa Barbara ya Majenda yenye urefu wa km 0.3, mradi wa Maji pagae, mradi wa kichomea taka, vyoo,na miundombinu ya Maji Nyambili, shule ya Semondari Wananchi, kikundi cha Mwafrika duka la dawa n.k.
Katika majumuisho Kanali Kolombo ameagiza miradi yote kuwa na nyaraka kwa kushirikiana vizuri na TAKUKURU sambamba na kufanya marekebisho yote yanayotakiwa katika miradi yote kabla ya kuwasili kwa Mwenge wa Uhuru wa Uhuru kuwasili.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.