Wataalamu kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Wataalamu wa dawati la msaada wa kisheria kutoka Halmashauri ya Kibiti Maafisa maendeleo ya Jamii, ,Maafisa kutoka ustawi wa jamii wadau kwa Pamoja leo tarehe 25 Februari 2025 wameanza utekelezaji wa kampeni ya msaada wa Kisheria wa Mama Samia katika Wilaya ya Kibiti.
Kampeni ya Msaada wa kisheria wa Mama Samia ( MSLAC) inayojiushisha na utoaji wa msaada wa kisheria imefanyika katika kata ya Kibiti ambapo Jopo la wataalamu hao lilitembelea Shule ya Sekondari Zimbwini, Shule ya Sekondari Dr.Samia-Lumiyozi Pamoja na eneo la Makaoni ambapo wamezungumza na wananchi wa eneo hilo.
Aidha zoezi hilo limejikita limejikika kutoa elimu na kutatua migogoro ya wananchi kwenye masuala ya ardhi,makosa ya jinai na madai, mirathi,malezi ya watoto, haki za watoto na ndoa
Kampeni ya msaada wa kisheria inatarajiwa kuendelea katika kata zote za Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti mpaka tarehe 5 Marchi 2025.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.