27.03.2024.
Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Kanali Joseph Kolombo akiwa amepokea na kukabidhi pikipiki 6 zilizotolewa na Wizara ya Mifugo kwa maafisa ugani wa Idara ya Mifugo.
Akikabidhi pikipiki hizo katika viunga vya Halmashauri hiyo, amewaagiza maafisa ugani hao kuzitunza na kuzitumia pikipiki hizo kwa matumizi yaliyokusudiwa huku akimpongeza Mhe. Rais Dkt. SSH na Wizara ya Mifugo kwa kuikumbuka Wilaya ya Kibiti na kupitia vitendea kazi.
Katika hafla hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti Ndg. Hemed Magaro amesema pikipiki hizo kwa upande wa Idara ya Mifugo zinakwenda kurahisisha kazi kwa kuwafikia wafugaji kwa wakati popote walipo ndani ya Wilaya ikiwa ni pamoja na kuongeza weledi wa utendaji.
Awali Afisa kilimo Mifugo na Uvuvi Wilaya Ndg. Simeon Waryuba alisema mapokezi ya pikipiki hizo yanakwenda kuziba pengo la kusuasua kwa utendaji katika Idara ya Mifugo hivyo, wanatarajia ufanisi wa kazi kuongezeka zaidi tofauti na ilivyokuwa awali.
Mara baada ya kukabidhiwa pikipiki hizo Maafisa Ugani wa Mifugo wameishukuru wizara kwa kuwapatia vitendea kazi kwani vitawasaidia sana katika kazi zao za kuwahudumia wafugaji na kuwafikia kwa haraka zaidi.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.