WAWILI WAKAMATWA KATIKA MSAKO HUO
MKUU wa Wilaya ya Kibiti Kanali Joseph Kolombo ameongoza msako wa kuwakamata wafugaji wavamizi katika Kitongoji cha Tarachu Kijiji cha Twasalie Kata ya Msala ambao huvamia na kulisha mifugo yao katika mashamba ya watu.
Kanali Kolombo akiwa amembatana na Uongozi wa Kata na Kijiji na Kamati ya Ulinzi na usalama katika msako huo, wamefanikiwa kuwakamata vijana wawili ambao ni vibarua wa wafugaji na kuwafikisha katika vyombo vya Dola .
Mara baada ya jopo lililofanya msako kutembea umbali wa takribani km 10 kuelekea katika kambi za wafugaji hao, walirejea kijijini na kukutana na wananchi ambapo aliwataka wananchi hao kuwa wavumilivu na kutoa ushirikiano wa kutosha kwa vyombo vya Dola Ili kufanikisha zoezi hilo kwani kilimo chao amekisikia.
"Niko hapa Leo kwa ajili ya kutafuta ufumbuzi wa kero zenu hususani wafugaji ambao huvamia mashamba yenu na kulisha mifugo yao, kilio chenu nimekisikia" Alisema Kolombo.
Vilevile kutokana na jiografia ya kisiwa hicho kuzungukwa na maji, Mkuu wa Wilaya Kolombo amewataka wananchi kuwa makini na kuchukua tahadhali ya wanyama wakali na waharibifu, wanapofanya shughuli zao za kibinadamu kandokando na ndani mto kwani changamoto ya mamba bado ipo.
Akitoa shukrani Kwa niaba ya wananchi wenzake ndg, Amiri Iddi Lyendeki amesema kupatikana Kwa mfugaji arimaarufu kwa jina la sura mbaya, kutasaidia kumalizika kwa kero hiyo Kwa haraka, kwani amefikia hatua ya kutishia watu maisha na kuhoji wakulima kwa Nini wamepanda mazao bila woga
Aidha Mwenyekiti wa Kijiji cha Twasalie ndg, Miraji Juma Mwingo amemshukuru Mkuu wa Wilaya kwa kufika jijijini kujionea hali halisi na kusema kwamba wananchi wamefarijika sana wamepata matumaini ya kudhibiti kero ya wafugaji kijijini hapo .
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.