Kwa mara nyingine tena kanisa la Christ Mandate la jijini Dar es Salaam limetoa msaada wa karatasi za kurudufu boksi 20 kwa ajili ya watoto waliowekwa kambi katika shule ya Msingi Kitundu baada ya shule zao kuzingirwa na maji ya mafuriko takribani miezi 3 iliyopita.
Akikabidhi msaada huo Mtumishi wa Mungu Malakain Joseph katika Ibada maalum ya watoto tarehe 22.06.2024 amesema kanisa lao lina mfuko wa kusaidia hivyo wamejitoa kuwasaidia watoto wa Kibiti waliopo Kambini.
Katika Ibada hiyo Mwakilishi wa Mkurugenzi kutoka Divisheni ya Awali na Msingi Mwl. Mariam Msofe, amelishukuru kanisa hilo kwa msaada huo muhimu kwakuwa utasaidia na kurahisisha maandalio ya wanafunzi wa darasa la 7 wanaojianda kufanya mtihani mwezi Septemba na majaribio ya mtihani wa kujipima kwa darasa la 4 ambao unatarajiwa kufanyika mwezi Novemba.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.