Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Kanali Joseph Kolombo amewasihi wakazi wa Kibiti na kada mbalimbali za kiutumishi kuendelea kuwa na mshikamano kwa maendeleo chanya ya Kibiti.
Kanali Kolombo amesema hayo Februari 9 katika Tamasha la Wanakibiti arimaarufu kwa jina la Kibiti day ambapo watumishi na wananchi kwa ujumla walijumuika na kufanya michezo tofauti tofauti asubuhi kabla ya sherehe ya jioni.
Mkuu huyo wa wilaya ambaye alikuwa ndiye Mgeni rasmi katika hafla hiyo Alisema lengo kubwa la kukutana ni kuweka umoja, mshikamano, kufahamiana na kubadilishana mawazo katika utendaji wa kazi.
"Lengo la kukutana katika michezo hii ni kuweka mshikamano, ndugu zangu wakazi wa Kibiti, endelezeni na kuimarisha umoja huu kwenye majukumu yenu" Alisema Kanali Kolombo.
Vilevile Kanali Kolombo amewashukuru wadau wote waliojitokeza kushiriki Tamasha Hilo kwani ni sehemu ya kuikuza Kibiti na kuleta maendeleo.
Katika Tamasha Hilo Katibu wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Kibiti Ndg, Zacharia Muhidini amewashukuru wote walioshiriki kufanikisha sherehe hiyo, huku Wahe. Madiwani wa viti maalum wakisisitiza kudumisha amani na utulivu jambo ambalo litasaidia Kibiti kusonga mbele.
Mbali na hayo amewataka wananchi wote kuzingatia na kujali Afya zao kwa kupima na kutambua Afya zao ili kuwa na nguvu kazi yenye utendaji madhubuti.
katika sherehe hiyo kulifanyika michezo ya kuvuta kamba, kukimbia na gunia, kufukuza kuku, kukimbia mbio fupi mita 100 ,mpira wa Pete, mpira wa miguu, mpira wa kikapu, na mpira wa wavu (volleyball) sambamba na kutoa vyeti kwa washindi wa kila mchezo.
Tamasha hilo lilihitimishwa kwa wadau wote kushiriki katika hafla ya usiku iliyofanyika katika viunga vya Shule ya Sekondari ya Wavulana Kibiti. Ilikuwa ni furaha, Watu walikula, kunywa na kupata burudani ya muziki huku wakipata wasaa wa kufahamiana na kubadilishana mawazo.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.