Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti imepokea ugeni wa shirika lisilo la kiserikali (NGO’S) kutoka nchini Marekani kupitia shirika la USAID ambalo hufadhili mapambano dhidi ya malaria THIBITI MALARIA kupitia Presidecial malaria initiative program chini ya Ofisi ya Rais Tanzania.
Akikaribisha ugeni huo Mganga Mkuu wa Mkoa wa Pwani na msimamizi mkuu wa mradi huo ambao utadumu kwa muda wa miaka mitano Daktari Gunini Kamba amesema kutokana na ukubwa wa tatizo la ugonjwa wa malaria anatamani na wilaya zilizosalia kufikiwa na Mradi huo.
Taasisi hiyo imewasili katika ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kibiti kwa lengo la kujitambulisha na kuona eneo ambalo mradi utatekelezwa kwani ni mradi mpya kwa Tanzania ambapo kwa mkoa wa Pwani upo katika Wilaya ya Kibiti na Mafia.
Vile vile wamesema kazi kubwa ya shirika hilo ni kuisaidia shughuli zote zinazohusiana na kudhibiti ugonjwa wa malaria na kwa Wilaya ya kibiti tayari wameshaanza kwa kutoa mafunzo ya usimamizi shirikishi wa malaria(MSDQI) kwa wataalamu wa afya watakaofanya nao kazi.
Mara baada ya kupokea ugeni huo Mkurugenzi Mtendaji Mohamed Mavura amesema amefurahia program hiyo kwa upekee wa kuchagua kibiti na mafia kwani mazingira yake yanafana na asilimia kubwa ya Wilaya hizo zimezungukwa na maji ukizingatia na mbu hujificha katika maeneo yenye maji maji na kuzaliana huku akiahidi kuwa tayari kutoa ushirikiano wa kutosha kuhakikisha mradi unatimiza malengo yaliyokusudiwa katika zoezi la kudhibiti na kukomesha ugonjwa wa malaria Kibiti.
Hata hivyo Mavura amesema tafiti nyingi za malaria zimefanyika bila ya mafanikio ni tumaini lake mradi huu wa THIBITI MALARIA utakuwa suluhisho katika ukanda wa Pwani kusini ambako malaria ni tatizo hususani kibiti kwa kawaida mvua hunyesha kuanzia mwezi 9-4 mfululizo jambo ambalo halikwepeki katika kutengeneza mazalia ya mbu.
Aidha Mganga Mkuu wa Wilaya Daktari Elizabeth Oming’o amesema amefurahishwa na ujio wa mradi huo kwani utakuwa mkombozi kwa Wilaya ya Kibiti ambapo katika magonjwa kumi ambayo wagonjwa hufika kutibiwa malaria inaongoza kwa kuwa na wagonjwa wengi zaidi mfano katika Kata ya Mtawanya Nyamisati n.k .Na kampeni hiyo itasaidia kutoa huduma sahihi katika Wilaya ya Kibiti na Mafia ambako mradi utatekelezwa.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.