"Ndugu zangu wanakibiti, wanasiasa wenzangu na watendaji, tusaidiane kuhimiza na kutekeleza majukumu yetu, hasa kupima ardhi ili kuvutia wawekezaji katika Halmashauri yetu" Alisema Mhe. Chaurembo, Mwenyekiti wa Halmashauri, Katika kikao cha baraza la kawaida ya robo ya pili ya mwaka. Katika swala la uwekezaji na utayarishaji wa mazingira yake, yatupasa kushikamana sote, wanasiasa na watendaji aliongeza.
Sisi wana Pwani Rais wetu Mhe. John Pombe Magufuli ametupa heshima kubwa, kuwa Mkoa wa viwanda hivyo niwajibu wetu kulipokea hilo kwa vitendo. Niombe Wananchi na Diwani wa Dimani nasisi sote kumaliza mapema swala la Kijani Kibichi katika kijiji cha Penda, ili waanze kufanya shughuli zao na kuleta tija kwa Halmashuri yetu.
Aidha, katika Baraza hili Mhe. Mkuu wa Wilaya akitoa taarifa za serikali alisema "Hakuna mahala popote palipo zuiliwa wananchi kuchangia elimu" Niwaombe kulipokea jambo hili kwa uzuri wake na kulitendea sawia na makusudio ya viongozi wetu. Kilicho zuiliwa nikuwaingiza waalimu katika kupokea na kuhamisisha michango hiyo, aliongeza Mhe. Kiffu.
Mhe. Mwenyekiti kupitia Baraza lako hili tukufu niombe tuu waheshimiwa Madiwanai wetu kuhamasisha wananchi katika maeneo yao katika kuchangia huduma za elimu na kusimamia wenyewe uratibu wake, na kwa kufanya hivyo tutakuwa tumeshiriki kikamilifu katika utekelezaji wa dhana hii.
Napia kabla sijamaliza tarifa yangu niombe kusema kuwa "swala la usimamiaji na uhamasishaji wa mapato ya Halmashauri hili si la mtu mmoja, bali sisi sote kwa nafasi zetu"
Hivyo basi niombe kuongezeka kwa weledi na ufatiliaji ilikufikia malengo yetu kwa wakati na kujiepusha na hatari za kufutwa kwa Halmashauri yetu. Kwani nikiwa kama mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama nasema sasa tuko salama na hakuna kizingizio, hivyo niseme tuu hatuna kisingizio bali tufanye kazi. Asanteni.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.