USINGIZI WA AMANI UNAOLALA WEWE NI MATUNDA YA JUHUDI ZA MASHUJAA WETU
Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti imeungana na Wilaya nyingine nchini katika Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa Leo tarehe 25 Julai ambayo hufanyika Kila mwaka Kama ilivyo desturi ya nchi yetu ambapo hutoa fursa ya kuwakumbuka mashujaa wa Tanzania waliojitolea maisha yao kwa ajili kupigania nchi yetu.
MKUU wa Wilaya ya Kibiti, watumishi wa Halmashauri, Taasisi mbalimbali, vyama vya siasa na dini wameadhimisha siku hii adhimu Kwa kufanya usafi wa Mazingira kituo cha afya kibiti.
Vilevile katika maadhimisho hayo Kanali Kolombo amesema sherehe hizi hufanyika ikiwa ni kumbukizi ya waasisi wetu Ili kuweza kuwakumbuka Mashujaa waluojitoa mhanga Kwa ajili ya kuitetea nchi yetu na kuiletea Amani.
" Tuko hapa kuwakumbuka Mashujaa waluojitoa mhanga Kwa ajili ya kuitetea nchi yetu, Daima tukumbuke kwamba Usingizi wa Amani tunaolala leo ni matokeo ya jitihada za mashujaa wetu, waliopoteza uhai wao katika kupigania Amani ya nchi yetu" Alisema Kolombo.
Hata hivyo Kanali Kolombo amewasisitiza wananchi kuona umuhimu wa kulinda na kuitunza amani tuliyonayo iliyopiganiwa na Mashujaa Hawa.
Aidha Mwakilishi wa mashujaa Wilaya ya Kibiti Joseph Milanzi ambaye alipigana vita ya Uganda mwaka 1978 - 1979 amefarijika kwa ngazi ya Wilaya kuadhimisha kumbukizi hiyo huku akiwapongeza washiriki wote kushiriki kumbukizi hiyo muhimu.
" Nimefurahi, nimefarijika Sana kwa kutujali na kuona thamani yetu Mashujaa wa Tanzania" Alisema Mstaafu huyo wa Jeshi Shujaa Joseph Milanzi.
Maadhimisho haya maalum hufanyika kitaifa katika Jiji la Dodoma, ambapo katika Mkoa wa Pwani yameadhimishwa katika viunga vya ofisi ya mkoa wa Pwani.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.