HALMASHAURI YA KIBITI YAPATA CHETI CHA PONGEZI
Machi,08 kila mwaka hufanyika maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani,kwa mwaka 2021 kimkoa maadhimisho haya yamefanyika Wilaya ya Mkuranga katika Kata ya Kimanzichana na mgeni rasmi kwenye maadhimisho haya alikuwa mkuu wa mkoa wa Pwani mhe.Mhandisi Evarist W. Ndikillo.
Kwenye kuadhimisha siku hiyo muhinu Duniani,Wanawake wengi walijitokeza wakia wamevaa sare zilizopendeza zikiwa zinatambulisha umoja wao ama vikundi vyao mbalimbali vya ujasilia mali ambavyo vingi vimepatiwa mikopo na serikali katika kuhakikisha wanakwamuliwa kiuchumi.
Aidha,kwenye maadhimisho hayo Halmashauri ya KIbiti ilikabidhiwa cheti cha pongezi kwa kushika nafasi ya pili miongoni mwa Halmashauri tisa(9) zilizopo mkoa wa Pwani, Kwa kutekeleza vyema shughuli za uwezeshaji Wanawake kiuchumi katika utoaji wa mikopo katika mwaka wa fedha 2019/2020.
Pongezi nyingi zimwendee Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kibiti Ndg Mohamed I. Mavulla pamoja na timu nzima ya wataalam kwa kutekeleza vyema kanuni ya utoaji wa mikopo ya asilimia kumi kwa vikundi vya Wanawake,Vijana na watu wenye ulemavu kama ilivyoelekezwa na Bunge.
IMETOLEWA NA KITENGO CHA TEHAMA NA UHUSIANO HALMASHAURI YA WILAYA YA KIBITI
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.