KIBITI YATIKISA PWANI ZAO LA KOROSHO
KATI YA KILO 258,955. ZILIZOUZWA 222,340. ZIMETOKA WILAYA YA KIBITI.
Mnada wa 9 na wa mwisho wa Korosho msimu wa 2021-2022 Mkoa wa Pwani umefanyika Wilaya ya Kibiti ambapo jumla ya kilo 258,955.zimeuzwa ambapo katika mauzo hayo kilo 222,340 zinatoka Wilaya ya Kibiti.
Katika mnada huo jumla ya kilo 11,092 zilizouzwa ni za daraja A na kilo 247,863 ni za daraja B,ambapo Bei ya wastani ya kuuzia daraja A ni 1520 wakati daraja B ikiwa ni 1202.2 na kwa pamoja wakulima wamekubali kuuza Kwa bei iliyopitishwa.
Vile vile Meneja wa Corecu Mkoa wa Pwani Hamis Mantaleo amesema katika minada yote 9 iliyofanyika msimu huu, kiwango cha ubora wa Korosho kimeongezeka kutoka 72 -96.5 ambapo mkoa wa Pwani Kwa ujumla umeuza kilo 10,683,796 ,kati ya hizo korosho kilo 10,311,436 ni za daraja la kwanza sawa na asilimia 96.5 huku kilo 373360 ni za daraja la pili sawa na asilimia 3.6.
Kwa mujibu wa Takwimu za mauzo ya korosho msimu wa 2021/2022 Wilaya ya kibiti imeendelea kuongoza uzalishaji wa korosho ambapo kati ya kilo 10,683,796 zilizouzwa kilo 6,112,324 zinatoka Wilaya ya kibiti ambazo ni sawa na asilimia 57.2 wa korosho zote za mkoa wa Pwani.
Aidha Afisa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Wilaya ya Kibiti ndg Bwenda Ismail Bainga amesema uzalishaji wa korosho na ufuta Wilaya ya Kibiti utaongezeka kwa sababu wakulima wameridhika na usimamizi mzuri wa mauzo na jinsi uongozi unavyofanya jitihada za kuwafikia wakulima vijijini.
Kwa upande wa korosho uzalishaji umeongezeka kutoka kilo 3,713,163 mwaka 2016 hadi kufikia kilo 7,601,539 Kwa mwaka 2021/2022
Katika ufuta uzalishaji umeongezeka kutoka kilo 2,496,000 mwaka 2016 hadi kufikia kilo 9 ,060,286 kwa mwaka 2021/2022 ikiwa ni ongezeko kubwa.
Hata hivyo Wilaya ya kibiti inatarajia uzalishaji ufuta na korosho kuongezeka mara dufu, kwani Uongozi wa Wilaya umejikita kuweka nguvu kubwa ya kuhamasisha na kuhakikisha wakulima wanalima kilimo bora na cha kisasa kwa kufuata maelekezo ya wataalam jambo linalopelekea wawekezaji kuvutiwa kuwekeza katika Kilimo Wilayani humo.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.