NI WILAYA PEKEE ILIYOAANDAA MAADHIMISHO HAYA MKOA WA PWANI.
Walimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti wameungana na Walimu wengine duniani kusheherekea siku yao muhimu ambayo huanzimishwa kila mwaka ifikapo Oktoba 5 .
Hafla hiyo iliyoadhimishwa katika viwanja vya shule ya msingi Bungu imebeba maudhui yasemao WALIMU TUNAOWAHITAJI KWA ELIMU TUNAYOITAKA ambapo katika Mkoa wa Pwani ni wilaya ya kibiti pekee iliyoweza kuandaa sherehe hiyo.
Akiwasilisha maelekezo ya Mgeni rasmi Mkurugenzi wa ELIMU TAMISEMI Vicent Kayombo, Afisa Taaluma msingi ndg, Edwin Kayuwi amesema Mkurugenzi Kayombo amewaelekeza Maafisa elimu kuwapandisha Walimu wote madaraja wanayostahili ifikapo mwisho wa mwezi novemba, kuwalipa Walimu nauli na fedha za kujikimu ambapo katika hili Halmashauri ya Kibiti imekwishalitekeleza. Pia Mkurugenzi Kayombo amesema katika kukabiliana na suala la uchakavu na upungufu wa miundombinu ya shule, nyumba za Walimu , vyoo na vyumba vya madarasa zoezi la ukarabati linaendelea kutekelezwa kulingana na utengaji wa bajeji ya 2023/24 takavyoruhusu.
Mgeni rasmi wa hafla hiyo Mwl. Bakari Mtembo ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Taifa kutoka CWT Dodoma, amemsisitiza Mkurugenzi wa kibiti kuona namna nzuri ya kutumia mapato ya ndani kuweza kutatua chanamoto ya upungufu wa walimu kwani kuna baadhi ya Halmshauri nyingine zimefanikiwa kwa kutumia njia hiyio.
"Moja ya kazi zangu ni kufikisha changamoto za walimu kwa mwajiri wao, Mkurugenzi hebu angalia namna nzuri kutatua changamoto hizi kwa kutumia mapato ya ndani" .Alisema Kitembo.
Licha ya changamoto zilizopo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti Bw. Hemed Magaro, amewataka Walimu kufanya kazi kwa bidii na kujituma, kwani kupitia madai yao Serikali ni sikuvu inaendelea kutatua changamoto zao kadri fedha zinavyoingia bila kumwacha mwalimu yeyote.
" Itafika wakati malalamiko yote mliyonayo yatakwisha kwani tumeweka utaratibu mzuri na tumeshaanza kulipa kwa baadhi ya Walimu kwa kufanya uhakiki wa kila mwalimu ili kila mmoja alipwe kulingana na stajiki yake" Alisema Magaro.
Aidha Magaro amewataka Walimu kuendelea kusimamia suala la malezi shuleni kwa kujenga urafiki na watoto ili waweze kusema yanayowasibu majumbani na mashuleni, kwani watoto wengi wameharibikiwa sana kimaadili.
Akisoma risala Katibu wa Chama chama ya Walimu Wilaya ya Kibiti Mwl Crecencia Tindwa amesema, chama che ye wanachama hai 580 na wasio wanachama 402 kinaendelea kuhamasisha Walimu kuchapa kazi kwa bidii kwanza wakati wakiendelea kudai haki zao, kama KAULI MBIU ya Chama mwaka huu Wilaya ya Kibiti isemavyo, WAJIBU na HAKI.
Aidha Katibu Tindwa amesema kupitia CWT wanamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupunguza changamoto ya upungufu wa Walimu kwa kuajiri Walimu 384 wa shule ya msingi na Walimu 206 wa shule za sekondari wakati upungufu ujenzi wa vyumba vya madarasa na vyoo ukiendelea kupunguzwa kutokana na majenzi yanayoendelea katika shule nyingi kwa fedha za Serikali na mapato ya ndani.
Hata hivyo Katibu Tindwa amesema mbali na pongezi hizo Walimu Wilaya ya Kibiti wanakabiliwa na changamoto kubwa ya ukosefu wa nyumba za Walimu, uwepo wa kesi za Usimamizi wa majenzi kwa Walimu Wakuu, kushindwa kusimamia Taaluma kutokana na kuzidiwa majukumu pamoja na mrundikano wa madeni ya likizo, uhamisho n.k
Kupitia risala hiyo Walimu wameiomba Serikali kuwapunguzia walimu hao Wakuu majukumu, ili waweze kujikita na shughuli za ufundishaji zaidi kwani wao hawana utaalamu wa ujenzi, huku wakisisitiza kuwaongezea bajeti za ujenzi katika maeneo ya visiwani ( delta) kwani mazingira yao kwausafirishaji ni magumu.
Katika hafla hiyo Mbunge wa Jimbo la Kibiti Mhe. Twaha Mpembenwe amewatoa shaka Walimu akisema kero zao amezibeba na ataendelea kuzisemea mpaka atakapihakikisha changamoto zimekwisha. Pia amewataka Walimu kuandaa utaratibu wa kuwa wanakaa pamoja naye na kusema kero zao na kuepukana na dhana ya kuwa na maandamani ya utatuzi wa changamoto zao.
" Hakuna sababu ya kuandamana ndipo mpate ufumbuzi wa madai yenu, njooni tuongee, wekeni utaratibu wa kukutana, milango ya Mbunge iko wazi muda wote kwa ajili yenu" Alisema Mpembenwe.
Awali Mwenyekiti wa Chama Cha Walimu Mkoa wa Pwani Deogratius Mhini amewataka Walimu kuendelea kuimarisha ushirikiano baina ya CWT, Chama Tawala na Serikali kwani kiutendaji ni lazima kushirikiana, huku Katibu wa Chama Cha Walimu Mkoa Bi. Sekela Saimon yeye amewataka Walimu kuwa na nidhamu katika ufundishaji kwa kufuata maadili na kuwasisitiza kujiendeleza kielimu ili kuweza kujiongezea ubora na kwenda na wakati kidigitali.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.